Kifo ni kitu cha kawaida sana. Kila mtu ana siku zake za kuishi na zikiisha basi ni lazima afe tu hamna namna.
Ifike mahali sasa tukizoee kifo. Siyo mtu akifa, wengine wanashangaa utafikiri ni jambo geni kutokea.
Muhimu ni kujiandaa kwa ajili ya ufalme wa MUNGU maana hakuna ajuaye ni lini atakufa. Kila mtu aangalie njia zake, matendo yake, maneno yake na fikra zake na ajitafakari mwenyewe kama anampendeza MUNGU au la.
Huwa siwaongelei marehemu kwa ubaya, sio kwasababu tuu ya imani yangu kwa mtu ila sababu sijui hata pale ambapo Mungu aliwachukua walikuwa kwenye hali gani kiroho