MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wakati wengine wakiendelea kupiga kelele kuhusu uteuzi wa Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, yeye ameanza kutoa majibu ya vitendo kama alivyoahidi wakati akiapishwa na Rais Magufuli.
Prof. Mkumbo alisema, “Maisha yangu yote mpaka hapa nilipo nimetumia muda wangu mwingi kuhoji na kuuliza maswali hasa kwa serikali. Nimepata fursa sasa ya kushiriki kikamilifu, badala ya kuhoji nina kazi ya kujibu maswali ya serikali. Mheshimiwa Rais nakuahidi kuwa nitajibu hoja mbalimbali za serikali kwa nguvu zangu zote”.
Wananchi wa wilaya za Mkoa wa Tabora zinaelekea kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji katika maisha yao ambapo wananchi zaidi ya milioni 1.1 wa wilaya za Tabora watapata huduma ya maji kufikia 2019.
Huu ni mradi ambao utavuta maji kutoka ziwa Victoria.
Kazi ya msingi ya serikali ni kujibu hoja/changamoto kwa vitendo na siyo maneno pekee.
Hii ndiyo kazi tunayoitaka katika msingi wa dhana ya HapaKaziTu katika kuleta maendeleo ya haraka nchini.