Sema team Mwandosya na Lowasa sio mbeya wote Kuna majimbo mbeya walimgomea Mwandosya na Lowasa wake wakaipa CCM wakamwacha na Sugu wake na chadema yake mwandosyaMbeya tumeungana kupinga ukatili wa awamu hii....
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.
Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.
Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.
Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.
Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.
Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.
Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.
Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.
Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”
Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”
Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.
Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.
Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.
Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.
Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.
Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.
Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.
Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.
Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.
Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.
Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.
Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.
Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.
Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Huo uchumi umekuwa kwenye makaratasi au mifukoni mwa watanzania? Mkuu! Hebu basi jaribu kujibu kwa ujenzi wa hoja siyo ushabiki ambao hauna afya sana.JANA NILIANDIKA HAPA, HUYU ANAE SUPPORT WATU WASIO NA HESHIMA KWA VIONGOZI WETU HAFAI HATA KUWA MWENYEKITI WA BOARD YA CHUO KWASABABU HATAKI KUUNGA MKONO UZALENDO NA KAZI ZILIZO TUKUKA AMBAZO MH. RAISI AMEZIFANYA KWA MDA MFUPI ALIO KAA MADARAKANI, BAADHI YA KAZI HIZO NI ELIMU BURE, RELI YA STANDARD GAUGE, FLY OVERS, KUZUIA WIZI WA RASMALI ZA NCHI, NA KULETA NIDHAMU KWENYE TAASISI ZA SERIKALI, NA KUKUA KWA UCHUMI WETU WA TANZANIA, Prof. ANATAKIWA KUJIULIZA, YEYE TANGU AWE MWANASIASA TUNAMKUMBUKA KWA LIPI? WATU KAMA SUGU WANAWASAIDIA NINI WANANCHI WA MBEYA?? KAZI YAO NI KUITUKANA SERIKALI TU, HAPO CHUONI NASIKIA ANA PROPAGATE UKABILA TU, HAKUNA ANACHOKIFANYA? KAMA KUNA MTU ANAFANYA KAZI HAPO ATUAMBIE AMESHA FANYA NINI CHA MAANA TANGU ATEULIWE?? AU ANAKULA POSHO NA MSHAHARA WA BURE?? HALAFU AMETEULIWA NA MPENDWA WETU RAISI, HUYOHUYO ANASUPPORT MATUSI YA AKINA SUGU?? SUGU NI RAIA KAMA ALIVYO RAIA MWINGINE ANAWAJIBU WA KUHESHIMU VIONGOZI NA KUFUATA SHERIA ZA NCHI, KAMA HUYO ANASABOTAGE SERIKALI, AHAMIE HUKO CDM ILI TUJUE KUW YEYE SIYO KADA MWENZETU WA CCM. HATUTAKI WANAFIKI NA WAFITINI.sina shaka kama prof haelewi nini maana ya rule of law.
Acha kukariri wewe umekuwa sasa!! Kama ni tusi si useme ni tusi gani?Insulting language 89(1) penal code. Kosa ambalo lilithibitishwa na mahakama bila shaka yoyote. Nyumbu wee
Sasa mnacholalamika ni nn hasa?mwandosya kumuunga mkono sugu au mwandosya kushindwa mara2 kura za maoni? Kuna watu wameshindwa mara kibao kura za maoni kuliko mwandosya ujue au tuwataje?Mwandosya kafanya kitu gani cha kukumbukwa kwenye utumishi wake katika taifa hili?? Hata CCM walishamkataa amegombea mara mbili kwenye kura za maoni ya uraisi lakini hakupata kitu!! Sasa uprofesa wake unatusaidia nini sasa?? Ana stress za kushindwa kwenye kura za maoni mara mbili. Aende huko hatusaidii kitu kama Chadema wanafikiri atawasaidia wampendekeze kugombea uraisi 2020 apambane na Raisi Magufuli tuone nani zaidi.
WatajeSasa mnacholalamika ni nn hasa?mwandosya kumuunga mkono sugu au mwandosya kushindwa mara2 kura za maoni? Kuna watu wameshindwa mara kibao kura za maoni kuliko mwandosya ujue au tuwataje?
Na Jumanne Lutengano Majoka
Mjasiriamali Mbeya Mjini.
Hakuna mashaka kuwa mapokezi ya bashasha na kauli aliyoiandika Prof. Mark Mwandosya katika ukurasa wake wa Twitter baada Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” kuachiwa kwa msamaha wa Rais hapo jana anaungana na kauli ya Sugu mwenyewe kuwa adhabu aliyoipata kwa kumtusi Rais ilikuwa ni kifungo cha kisiasa.
Kwa Prof. Mwandosya na Sugu mwenyewe ni vizuri kujiepusha na upotoshaji huu. Sugu alifungwa kwa kosa la jinai na hivyo alikuwa mfungwa wa kosa la jinai na sio mfungwa wa kisiasa kama anavyodai.
Mfungwa wa kisiasa ni mtu aliyefungwa jela kutokana na kujihusisha na shughuli ama imani za kisiasa. Hapa ndipo mtu kama Nelson Mandela anaitwa mfungwa wa kisiasa.
Lakini Sugu sio mfungwa wa kisiasa, Sugu ni mhalifu, alifanya makosa ya kuvunja sheria za nchi kwa kumtukana Rais. Hata utambulisho wake anaitwa Mfungwa namba 219/2018 na sio Mfungwa wa Kisiasa namba 219/2018 kama anavyodai na kama Prof. Mwandosya anavyounga mkono.
Hizi ni siasa za kipuuzi na zinapoungwa mkono na mtu mwenye utumishi kwa nchi kama Prof Mark Mwandosya inatia wingu zito na inavunja heshima.
Nimejiuliza sana kuhusu lengo la Prof. Mark Mwandosya kumpokea Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” aliyetolewa jana Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais na ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter. Tena Prof. Mwandosya kafunga safari hadi nyumbani kwake Sugu kumpokea na kuandika alichoandika.
Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.
Na akaendelea kwa kimombo “Congratulating Hon.Joseph Mbilinyi-right after graduating from Ruanda Prison Mbeya”
Baadaye Sugu nae kapost picha kwenye Instagram wakiwa wamekaa na Prof Mwandosya nyumbani kwake Sugu na Prof Mwandosya akinywa juisi na kaandika “Nikiwa na Prof. Mwandosya nyumbani kwangu leo. Asante kwa maneno ya busara na ujasiri ulionipa leo na hata ulipokuja kuniona gerezani”
Ukiunganisha nukta za kauli za Prof. Mwandosya na Sugu haileti mashaka kuwa wanaongea lugha moja kwamba Sugu ni mfungwa wa kisiasa na wanataka kuaminisha umma kuwa Sugu alionewa kwa adhabu ile.
Niseme hivi kwa Sugu kutoa kauli hizo haina shida kwa sababu kwa namna yoyote baada ya kukumbwa na adhabu ile ilitarajiwa kuwa atataka kuitumia kwa manufaa ya kisiasa, lakini kwa Prof Mwandosya kuna ukakasi.
Kuna ukakasi kwa sababu Prof. Mwandosya ni Mwanachama wa CCM na aliyetukanwa na Sugu ni Mwenyekiti wake. Kwa alichokiandika Prof. Mwandosya ni wazi kuwa anaamini Sugu alionewa na anamtia moyo kuwa amefuzu chuo cha uanasiasa katika gereza la Ruanda. Anaamini kuwa Rais Magufuli alistahili kutukanwa vile na Sugu na hakubaliani na adhabu aliyopewa na mahakama kwa mujibu wa sheria.
Prof. Mark Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambacho awali kilifanya kazi ya kutengeneza makada na sasa kinafundisha kozi mbalimbali za uongozi, siasa, uchumi n.k. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chuo hiki na Rais Magufuli ambaye ametukanwa na Sugu na hakukataa uteuzi huu.
Prof. Mwandosya ni Waziri mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne na ni mtu aliyejitokeza mara mbili kutaka ridhaa ya wana CCM ili agombee kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio.
Kwa mazingira hayo hapo juu, Prof. Mwandosya angepaswa kuwa makini na kauli zake na ikiwezekana aamue moja ama kujipambanua kuwa yeye sasa anaunga mkono siasa za upinzani na kujihusisha na upinzani kwa uwazi ama kuchunga kauli zake. Aamue ama kuwa moto ama kuwa baridi aache double standards.
Ni jambo linalokanganya kwamba anatumikia cheo alichopewa na Rais Magufuli, anatibiwa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli na ni mwanachama wa chama kinachoongozwa na Rais Magufuli halafu anamuunga mkono mtu anayemtukana Rais Magufuli.
Na hii sio mara ya kwanza kwa Prof. Mwandosya kufanya double standards hizi. Mwaka 2015 alipokosa kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM aliibuka na kumshambulia Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akipinga mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Ilitushangaza wengi kwa sababu Prof. Mwandosya alipaswa kujua kwa nini chama kiliamua kumteua Magufuli na angepaswa kuelewa hata manufaa ambayo chama kimeyapata maana ni wazi kwamba kama wangepitishwa waliokuwa wanatajwatajwa pengine chama kingepoteza kwenye uchaguzi mkuu.
Nakusihi Prof Mwandosya kama una mahaba na upinzani hamia huko, mimi kama Mtanzania ninayeamini katika utawala wa sheria, na ninajitahidi kupambanua mambo kwa maslahi ya Taifa naona unachokifanya sio sawa, kama wanavyosema vijana inawezekana unataka kupata Kiki au uendelee kupata umaarufu wa kisiasa, lakini kwa heshima yako hili unalolifanya unakuwa Kivuruge.
Sipendezwi na aina ya siasa zinazofanywa na upinzani na ni miongoni mwa watu wanaopenda kuwepo upinzani wenye tija na sio upinzani unalivuruga Taifa kama huu tulionao Tanzania. Tuna upinzania ambao hauna dalili za kushika dola na hauna tija.
Alituhumiwa hivyo kutokana na namna alivyofanya siasa zake mwaka 2005 alipochuana na Jakaya Kikwete katika ngazi ya chama. Kwa wakati ule zilikuwa ni nguvu za mtandao. Mtandao wa Prof. Mwandosya ulibeba sura ya kikanda zaidi.
Nionavyo mimi kama Prof. Mwandosya hatojisahihisha ni wakati sasa wa Rais Magufuli kumuengua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni. Aachwe huru ili afanye siasa za upinzani kwa uhuru zaidi, aungane na Sugu na wanasiasa wengine wa upinzani kufanya siasa bora zaidi.
Prof Mwandosya aamue kuwa baridi au kuwa moto.
Mimi ni mwananchi wa Tanzania
Naitwa Jumanne Lutengano Majoka.
Kwa ambao hamjasoma alichopost Prof. Mwandosya, kapiga picha akiwa na Sugu nyumbani kwa Sugu kaandika hivi nanukuu “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Mhe.Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa,Gereza la Ruanda,Mbeya.Kutofautiana vyama,itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui.Mungu Ibariki Tanzania.
Hapa tulipofikia tunahitaji wahuni, maniga na mabedui wa kutosha ili tutoke kwenye huu mkwamo!!Sugu ni niga, bedui, mhuni