Prof. Mark Mwandosya ni mpotoshaji

Aisee. Mwambie Mwenyekiti amfukuze chamamani. FAHAMU kuna makabila Tanzania wanapendana no matter what na mfano ni wa kutoka Mbeya, Kilimanjaro, Mikoa ya Wasukuma, Kanda ya Ziwa hapa Mara na Kagera. Hawa watu wana asili ya kwao. Na hata sasa inajidhihirisha wazi. Hivyo huwezi kuongelea la Sugu Mbeya. Na nikuambie kisiasa lina impact kubwa mno kwa wanambeya ninaowafahamu. Hapo kuna tension kubwa na Chama Changu ninawasihi muwe makini na msikurupuke.
 
Kwahiyo kwa maelezo yako meeengi hivyo unataka tukuamini wewe?
 
Unaandika sana lakini hakuna cha maana ulichoandika.
Ungeelewa Muktadha wa swala zima lilivyokua usingeandika huu utumbo hapo juu.
Maneno aliyoyatoa Sugu mpaka akakamatwa hakuyatoa Akiwa Kanisani, Bar au Mpirani. Maneno hayo aliyatolea kwenye Jukwaa la Siasa, alikua akifanya Siasa ndio maana akakamatwa na Kufungwa.

Pili Unamshambulia Mwandosya kwa mambo ambayo hayahusiani na huu Muktadha. Ugonjwa wake, siasa alizofanya mwaka 2005, Uenyekiti wake wa Bodi havitengui wala kuhusiana na kile alichokisema wakati akimpokea Sugu.
 
Kwahiyo unataka tukuone wewe ni zaidi ya Prof. Mwandosya kwa uharo uliou-post hapa? Wenye kumwelewa Prof. Mwandosya tulishamwelewa. Vijineno vyako haviwezi kutufanya tufute tulichokisoma ktk maneno ya Prof. na Sugu mwenyewe kuhusiana na saga hili.
 


Sasa wewe Mbona umemdhalilisha prof kwa kutaja ugonjwa wake ns kusema sijui ana vyuma na hakuna atakayekupeleka mahakamani. Na pia umemwita MTU mzima mpotoshaji - matusi makubwa sana.
Na unamchagulia cha kuamin na kuandiia, inamchagulia marafiki- huo ni udhalilishaji na matusi kwa MTU mzima.
Alivyopelekwa nje kwa matibabu ilikuwa hisani au kwa mujibu wa sheria?
Huo uenyekiti wa Bodi ya chuo alituma barua ya maombi???
Kwa siasa za Tz ambazo wananchi wanafuata na kuamin watu badala ya itikadi, CCM inamwitaji Mwandosya huko nyanda za juu kusini kuliko anavyohiitaji ( angalia ya kanda ya kadkazini na ENL na kilichotokea katika election ta 2015).
Kwa hiyo utulie kijana, wenye busara kwenye chama watajua namna ya kuliweka kibusara zaidi.
 
Sio jambo jema kumpangia Prof Mwandosya aina ya marafiki. Ni mtu mzima, msomi na anazo akili timamu.

Kulitambua hilo ndio maana halisi ya ukomavu wa kisiasa na hata katika masuala ya mahusiano ya kibinadamu.
 
Wako wengi haina yake Prof Mwandosya ambao kwa kutoshwa na Serikali inayongozwa na Dr Magufuli, hawafichi hasira na chuki zao. Haitomsaidia katu.
Aliposhindwa kuteuliwa kugombea uraisi kupitia CCM jina lake lilipokatwa hasira zake zilianzia pale
 

Tuambie ni akina nao hao waliofanya ya kufaa na ni yepi??
Usiwe na za mkizi, kutofautiana mtazamo sio uadui?? Chuki ya nini?
Why unune wenzio wanapofurahia ndugu yao kumaliza kifungo??? .
Tulis tafakari ni sababu gani zinakufanya utoe povu kiwango hiki??? Why??
 
prof Mwandosya ana akili kukuzidi wewe mtoa mada, tulia kimya
 
yaani nyie kiongozi yeyote anayeongea ukweli ni adui wa Rais sasa mbona kama vile tutakuwa ni Taifa la ndio mzee jambo ambalo sio sawa, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake kadiri ya utashi wake, nami nakubaliana sana na prof na wala musimkashifu mzee wa wakati anajua alichozungumza
 
Ninasikia hata Mbeya hajafanya kitu chochote. Mbeya vijana wengi ninasikia ni wasomi na ni jobless, naambiwa hajafanya chochote na ni mselfish. Mbeya wanamkumbuka Mwakangale, Mwambulukutu, Mwaikambo kidogo kwa mbali sasa wanatumaini na Dr Tulia. Mwandosya ni mtu wa Visasi na Hana msaada Wowote kwenye Chama au serikali Mbeya. Ukiona kijana wa Mbeya yupo kwenye nafasi yoyote Jua kajipigania na si kwa sababu ya Mwandosya
 
Sio jambo jema kumpangia Prof Mwandosya aina ya marafiki. Ni mtu mzima, msomi na anazo akili timamu.

Kulitambua hilo ndio maana halisi ya ukomavu wa kisiasa na hata katika masuala ya mahusiano ya kibinadamu.
Kuna umri ukifika ukastaafu Ni vizuri kuendelea na Mambo mengine Kama kulea wewajukuu nk sio kuendelea na Yale uliyostaafia .Mwandosya umri umeenda Bado anaota siasa na wazee wenzie akna Sumaye
 
Aliposhindwa kuteuliwa kugombea uraisi kupitia CCM jina lake lilipokatwa hasira zake zilianzia pale

Mtasema mengi.Siku hazigandi , sugu katoka gerezani. Hata ingekuwa miaka 20 ingeisha tu.
Msifikiri kila MTU alifurahia kushitakiwa na hatimaye kufungwa kwa Sugu.
 
Hakuna haja ya kutetea sana uhalali wa kesi na hukumu ya Sugu. Dunia inajua na Watanzania wote wanajua juu ya kesi ya Sugu, mwenendo wa hakimu, polisi na upande wa mashitaka.

Vv
 
Soma vizuri sababu za kisheria za Nelson Mandela kufungwa. Kwa makaburu, Mandela alifanya na kufungwa kwa makosa ya jinai. Actually, kwa definition yako ya wafungwa was kisiasa hakuna hata mmoja katika uliowataja au unaowajua mbao ni wafungwa wa kisiasa.....wengi ya tunaowajua walifungwa kwa makosa ya jinai! Kote shida huwa ni tafsiri ya hizo jinai....watawala huweka sheria (zisizokubalika, za kibaguzi), ukikataa hiyo ni jinai tu. Hakuna katika sheria zetu na za wengine adhabu za kifungo kwa "makosa ya kisiasa". Ukiona mtu kafungwa, ujue ni jinai tu kwa mujibu wa watawala.

CCM wakitukana wapinzani sio jinai ni siasa, wapinzani wakitukana watakatifu wa kijani ni jinai!
 
Lumumba kuna tatizo kubwa. Yatakiwa uwe na ujivunie kuwa mnafiki. Uwe msharika wa ibada ya kumsifu na kumshangilia Mfalme Jiwe kwa kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…