Prof. Lipumba na mtazamo potofu juu ya dhana ya ufisadi

Makombeni10

Member
Jul 29, 2015
34
64
Juzi Tarehe 11/5/2017 Lipumba, John Cheyo, Agustino Liyatonga Mrema na wengine wachache waliojinasibu na kujipambanua kuwa ni viongozi wa vyama vya upinzani nchini walihudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na mwenyeji wake Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam. Zuma amekumbwa na upinzani na shinikizo kubwa nchini mwake kutoka ndani ya Chama chake cha ANC na vyama vya Upinzani vya EEF-JULIUS MALEMA na Democratic Alliance (DA)- kutokana na UFISADI mkubwa wa MALI ZA UMMA kwa matumizi yake binafsi na matumizi mabaya ya madaraka ya Urais. UFISADI wa Zuma umethibitishwa na Mahakama KUU nchini mwake na kuamuriwa kurejesha Fedha hizo alizozichota katika Hazina ya nchi kujenga kasri binafsi kijijini kwake.

Sote kama Watanzania tunakubaliana na juhudi na mchango mkubwa wa Chama cha ANC katika kupigania ukombozi na kupiga vita UKABURU na UBAGUZI wa rangi nchini AFRIKA YA KUSINI chini ya NELSON MANDELA na wapambanaji wenzake wote akiwemo Jacob Zuma. Zuma amekwenda kinyme na DHAMIRA na MALENGO ya kupigania UKOMBOZI HUO na badala yake kujilimbikizia mali binafsi na matumizi mabaya ya dhamana aliyokuwa nayo. Vyama vya EEF na DA haviruhusu hata Zuma kulihutubia Bunge na kumtaka aondoke madarakani. Wananchi wapo barabarani kila uchwao wakimtaka aondoke madarakani. Askofu Desmond Tutu mpiganaji mashuhuri wa ANC ameungana na wasouth kumtaka Zuma aondoke madarakani.

Kiongozi unapoamua kupiga vita uovu, ufisadi, dhulma na aina yeyote ile ya ukandamizaji na uonevu lazima usimamie misingi hiyo kwa mapana yake (Universal Principal). Huwezi kupiga vita Ufisadi ukitendwa Ilolanguru alafu ukabariki Ufisadi kama huo ukifanywa mahala pengine nje ya Ilolanguru. Hapa ndipo panapojitokeza mashaka na uthibitisho wa UKIBARAKA NA KUTUMIWA NA WATAWALA. Mwalimu Nyerere pamoja na mapungufu yake alisimamia misingi hiyo kwa viongozi wote alioamini kuwa wanakwenda kinyume na misingi ya haki za binaadamu na kujivisha Joho la udikteta na umwagaji wa damu za raia wasio na hatia. Hakukubali kukaanao meza moja na hata kuwapa mikono kwa kusalimia nao.

Lipumba kuhudhuria dhifa ya Rais Jacob Zuma mwenye matatizo makubwa ya kushindwa kusimamia utawala bora na wa sheria nchini mwake, ameshindwa kulinda Tunu zile anazoziita Lipumba za Maadili, Utu, Uadilifu, na Uzalendo nchini mwake. Hapa Lipumba amejifedhehesha sana na kujipambanua kuwa si kiongozi wa viwango Kitaifa na kimataifa, amedhihirisha UNDUMILAKUWILI wake “Double Standard’’ unajinasibisha kupinga Ufisadi wa ndani lakini unaukumbatia Ufisadi wa nje. Lipumba yule tuliyemjua awali siyo huyu wa leo. USALITI unazidi kuongezeka wigo. Sio ndani ya CUF pekee. Sasa USALITI umevuka mipaka mpaka umefika kwa wananchi SA, vijana wanaita BONDENI kwa Mzee MADIBA. LIPUMBA KAWASALITI WAPIGANIA HAKI WA SOUTH AFRICA.
 
"Tanzania hakuna mpinzani kweli hapa"

Mpinzani wa kweli alikuwaga "Mtikila peke yake"""

Hivyo kumkataa lipumba kama sio mpinzani kweli na kumkubali mbowe au lowassa kama wapinzani wa kweli"

Ni sawa sawa na kwenda mganga huku ukipinga ushirikina
 
Mku ukiona Mtu mzima anajitoa ufahamu ujue huyo hana baraka tena ndani ya familia yake pamoja na jamii inayomzunguka kwa hiyo watu kama hawa katika mwisho wao ndio kama unavyowaona ktk picha

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Hivi bado mnamjadili Lipumba kwa kiwango hicho?Mbona mi namuona hana hata hadhi ya kujadiliwa kama Hamorapa?Kwa umri wake na mambo anayofanya unaona kabisa uwezo wa kufikiri ni mdogo sana!
 
Back
Top Bottom