Prof. Kitila Mkumbo: Serikali inavuruga vyuo vikuu

Ndg, unapaswa kujua kuwa vyuo vikuu hapa duniani haviendeshwi kama shule za msingi. Kuna uhuru wa mawazo. Na ili taaluma iendelee lazima kuwepo na mijadala na majadiliano mbalimbali ya kitaaluma.

Sasa wewe unaposema kuwa mijadala haina manufaa kwa kuonyesha kuwa awamu ya nne mijadala ilikuwa huru n.k lakini haikusaidia viwango vya elimu kukua, unapaswa kutambua kuwa kuna maswala mengine pia yanayoathiri ubora wa elimu ya vyuo vikuu.

Mijadala ni muhimu sana katika maendeleo ya kitaaluma. Wanazuoni wetu wanapaswa kuwa na uhuru wa kutoa michango yao kimawazo. Isitoshe mnaogopa nini mihadhara wa wanachuo? Tukiendelea hivi kuwazuia wanazuoni kujadili maswala yao ya kitaaluma wanapokuwa chuoni tunatengeza viongozi ambao watakuwa wakipewa mialiko UN, Zambia, AU n.k watakwepa kwa sababu ya kukosa uwezo wa kutoa hoja, lakini pia hawatakuwa na uwezo wa kutetea hoja zao dhidi ya mawazo kinzani.

Hii Ndiyo sababu ya kukwambia uyaache mambo ya kitaaluma kwa wanaoijua elimu ya chuo kikuu.
 
Mimi nahisi uongozi wetu wa sasa haujiamini, ndiyo maana unaogopa watu kuwa huru kujadili mambo, hii hali inataka iniaminishe pia kwamba kitendo cha Mkulu kutokwenda nje ya nchi katika mikutano mikubwa muhimu si kwamba anataka kupunguza ghalama tu bali pia hana uwezo wa ku-argue na vichwa vya nafasi yake katika forum za kimataifa.
 
Wewe utakuwa unahitaji consultant!!!!!
 
Kuna Mkuu Mmoja Aliwahi Kusema Humu, " Tunahangaika Kunyoosha Vivuli Vya Miti Wakati Iliyopinda Ni Miti Yenyewe".
Tutawalaumu Wasomi Wetu, Tutakejeli Elimu Zao Lakini Bado Haya Yote Ni Matokeo Tu Na Wala Sio Chanzo.
Cha Muhimu Kujiuliza Ni Je, Mifumo Yetu Ya Elimu Inasaidia Kutatua Changamoto Zetu Kama Taifa? Je, Wasomi Wanaotokana Na Mfumo/Mifumo Hiyo Wana Ujasiri Wa Kusimamia Na Kutekeleza Yale Yote Yenye Manufaa Na Tija Kwa Taifa?
 
Anashangaa nini wakati wanataaluma wameona dili ipo kwenye siasa na kujikomba kwa watawala?
 
Huyo naye anatafuta Kiki muulize Twaweza anafanya nini zaidi ya kupika tafiti
 
yaan mtu unasema kuwa kitila kaongea pumba et kisa siasa,jamani muwe na akili muda mwingine mtu akiongea jambo la maana mpeni sifa zake siasa baadae!!
Tatizo maprofesa wetu hawa ni wanafiki.
 

Sawa imeanza kumwingia
 
Bora kukaa kimya usijulikane msimamo wako . nawapongeza maprofesa wanaoamuwa kukaa kimya.
 
Unamwambia nani wakati uko kwenye system?Kwani hamjui nyie wasomi ndiyo hamna michango kwa jamii yetu?Ninyi ni wasomi lakini ni wasanii wa siasa.
Na hili ndilo litakalo tufanya maendeleo ya kweli tuyasikie kwa wenzetu tu.
 
kama mtu hayupo pamoja na wewe kimawazo sio mnafiki,tatizo watu wajiona kama hawajui kukosea
Tatizo Siyo kuwa pamoja kimawazo.msomi kama Kitila mkumbo lazima awe na msimamo na agenda zake anazopigania. Yani Lila mtu akisikia kitila anataka kuzungumza tayari unafahamu mwelekeo kwa kuwa unajuwa ni mtu wa mrengo upi.sasa Prof leo yupo hivi kesho vile hatumwelewi kwakweli anyway kwa sababu ni politician labda.
 
Nakubaliana na Prof Kitila katika hili, anayo hoja ya msingi kabisa. Lakini ni muhimu pia akakubali kwamba wasomi wenyewe, kwa maana ya vyuo vikuu vyetu, ndio vinastahili kubeba lawama kabla ya kuilaumu serikali. Zamani vyuo vikuu ndiko ambako kulitegemewa kuzalisha fikra zenye kusaidia taifa kwenda mbele zaidi, lakini leo vyuo vikuu navyo vimegeuka kuwa conduits za kufanikisha ajenda za kisiasa za kimakundi.

Kwa mfano, unapomwona msomi kama Dk Bana akihojiwa na chombo cha habari kuhusu jambo nyeti linaloihusu nchi, kabla hata hajaanza kuzungumza unajua atakachokizungumza. Lakini hata Prof Kitila mwenyewe amekuwa na tabia ya kuingilia na kuvuruga mijadala inayoelekea kuelemea serikali kwa lengo ambalo pengine analijua yeye mwenyewe. Hata 'timing' ya kuzungumzia mambo yanayozigusa siasa za nchi, inayofanywa na wasomi, imekuwa ikivunja mioyo ya watu na kuanza kuwaona baadhi ya wasomi kama wachumia tumbo tu wasio na lolote katika jamii.

Ni muhimu sasa kama akina Kitila wanafahamu "Umuhimu wa elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika" waachane na siasa uchwara za kimakundi zinazoendelea katika nchi hii, bali wasimame kama wasomi kwa kuwa kwa kufanya hivyo jamii itawaheshimu na serikali nayo itawaona ni watu wanaostahili "kuingiliwa".
 
alisema kuwa CUF ya lipumba itakuwa imara,mi nilimuelewa vizuri,kwamba kitakuwa chama imara ila si cha utetezi wa watanzania.yaan IMARA ILA KWA KUWA HAKIPO UKAWA.coz ndani ya kuwa wanaongozwa na chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…