Prof Kitila: Bado sijaelewa sera ya uchumi wa awamu hii

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jamvi
Salaam, amani iwe kwenu

Prof Kitila Mkumbo anaongea na Clouds tv hasa katika kuchambua uongozi wa awamu hii katika nyanja kadhaa, anasema serikali imenuna na wananchi pia wamenuna sana
kiuchumi, mambo yalioyumba ni pamoja na Watumishi wa umma na wafanyabiashara
Aidha amesema serikali inapaswa kuongezea nguvu katika sekta binafsi kuliko kutegemea taasisi za serikali katika kutoa huduma mbalimbali, pia suala la elimu bado hakuna falsafa ya elimu nchini, kuhusu huduma za afya bado haijawa vizuri vilevile kwa mwaka mmoja uliopita 2016 katika siasa vyama vya siasa vilibanwa na dola,kulikua hakuna uhuru wa kujieleza, amelinganisha na awamu zilizopita zote zilizopita.Wakati wa Mh Mkapa kulikua na proper mixed economy na uchumi uliimarika
zaidi, lakini bado hajamuelewa Mh Rais Magufuli yupo katika dhana gani ya uchumi aitha anafuata wa Hayati Nyerere, Mwinyi ,Mkapa ama Kikwete

katika suala zima la uchumi
Wakati wa Rais Mkapa alifanya kazi nzuri katika kuboresha uwekezaji aitha kulikua na stability ya kisiasa na kuvutia wawekezaji

Chanzo: Clouds TV
 
Wana jamvi, salaam

Prof Kitila Mkumbo anaongea na Clouds tv hasa katika kuchambua uongozi wa awamu hii anasema serikali imenuna na wananchi pia wamenuna kiuchumi, mambo yaliyoyumba ni pamoja na Watumishi wa umma na wafanyabiashara.

Aidha amesema serikali inapaswa kuongezea nguvu katika sekta binafsi kuliko kutegemea taasisi za serikali katika kutoa huduma mbalimbali. Vilevile kwa mwaka mmoja uliopita 2016, amelinganisha na awamu zilizopita hasa ya Mh. Mkapa kulikua na mixed proper economy na uchumi uliimarika zaidi lakini bado hajamuelewa Mh. Rais Magufuli yupo katika dhana gani ya uchumi, aidha anafuata wa Mh Nyerere, Mwinyi ,Mkapa ama Kikwete katika suala zima la uchumi.

Wakati wa Rais Mkapa alifanya kazi nzuri katika kuboresha uwekezaji na kulikua na stability ya kisiasa na kuvutia wawekezaji.

Chanzo: Clouds TV

Namfuatilia hapa ngoja wamlize kipindi ndio nitakuja na comments
 
Wana jamvi
Salaam
Prof Kitila Mkumbo anaongea na Clouds tv hasa katika kuchambua uongozi wa awamu hii anasema serikali imenuna na wananchi pia wamenuna kiuchumi, mambo yaliyoyumba ni pamoja na Watumishi wa umma na wafanyabiashara
Aidha amesema serikali inapaswa kuongezea nguvu katika sekta binafsi kuliko kutegemea taasisi za serikali katika kutoa huduma mbalimbali, vilevile kwa mwaka
mmoja uliopita 2016, amelinganisha na awamu zilizopita hasa ya Mh Mkapa kulikua na mixed proper economy na uchimi uliimarika zaidi lakini bado hajamuelewa Mh Rais Magufuli yupo katika dhana gani ya uchumi aitha anafuata wa Mh Nyerere, Mwinyi ,Mkapa ama Kikwete
katika suala zima la uchumi
Wakati wa Rais Mkapa alifanya kazi nzuri katika kuboresha uwekezaji aitha kulikua na stability ya kisiasa na kuvutia wawekezaji

Chanzo: Clouds TV
Hawa maprofesa waache kumsumbua JPM na nadharia zao vitabuni. Hapa Kazi Tu ndio dhana ya awamu hii, na matunda yake yanaonekana kwa wenye macho !
 
Asichoelewa kwenye uchumi wa " viwanda na uwekezaji" ni nin hasa... btw clouds wanamuhoji vipi mtaalam wa elimu na saikolojia mambo ya uchumi?
Kama mtanzania msomi wa ngaz ya juu na mwanachama mwandamizi wa ACT walitumika sana kushadadia 'utawala huu uingie madarakani"

Nakumbuka alivokuwa anashupalia 'Utafiti" wa twaweza...
Mwambieni atetee serikali aliyopigania kuiweka madarakani...
Na bado tuna imani na serikali yetu kwa asilimia tisini na sita nukta saba..

Mheshimiwa hawezi kumpa kila mtu cheo.......
 
Mlango mmoja wapo wa sekta binafsi na sekta ya umma kushirikiana,ni katika manunuzi ya umma.

Sheria ya manunuzi ya umma kwa sasa iko suspended,haitumiki,

Tanzania ina watu karibu au zaidi ya milioni 50, serikali imeajiri watu wasiozidi milioni moja na nusu, jibu liko wazi kwamba waliosalia katika milioni hamsini wamejiajiri na wameajiri.

Sasa hawa walioajiri na waliojiajiri katika sekta binafsi ambao Mimi nawakadiria kama milioni 30-40,unapowaandalia mkakati wa kuwatenga na kuwayumbisha unatarajia nini?

Nadhani sekta ya umma na binafsi ni kama mdomo na ulimi,mmoja akijifanya wa maana,asifikiri anamkomoa mwenzie,bali wataporomoka wote
 
Mlango mmoja wapo wa sekta binafsi na sekta ya umma kushirikiana,ni katika manunuzi ya umma.

Sheria ya manunuzi ya umma kwa sasa iko suspended,haitumiki,

Tanzania ina watu karibu au zaidi ya milioni 50, serikali imeajiri watu wasiozidi milioni moja na nusu, jibu liko wazi kwamba waliosalia katika
milioni hamsini wamejiajiri na wameajiri.

Sasa hawa walioajiri na waliojiajiri katika sekta binafsi ambao Mimi nawakadiria kama
milioni 30-40,unapowaandalia mkakati wa kuwatenga na kuwayumbisha unatarajia nini?

Nadhani sekta ya umma na binafsi ni kama mdomo na
ulimi,mmoja akijifanya wa maana,asifikiri anamkomoa mwenzie,bali wataporomoka wote

:(
 
Mlango mmoja wapo wa sekta binafsi na sekta ya umma kushirikiana,ni katika manunuzi ya umma.

Sheria ya manunuzi ya umma kwa sasa iko suspended,haitumiki,

Tanzania ina watu karibu au zaidi ya milioni 50, serikali imeajiri watu wasiozidi milioni moja na nusu, jibu liko wazi
kwamba waliosalia katika

milioni hamsini wamejiajiri na wameajiri.

Sasa hawa walioajiri na waliojiajiri katika sekta binafsi
ambao Mimi nawakadiria kama
milioni 30-40,unapowaandalia mkakati wa kuwatenga na kuwayumbisha unatarajia nini?

Nadhani sekta ya umma na
binafsi ni kama mdomo na
ulimi,mmoja akijifanya wa maana,asifikiri anamkomoa mwenzie,bali wataporomoka wote

Afadhali prof maji marefu angekuja na suluhisho

:(
 
Wana jamvi
Salaam, amani iwe kwenu

Prof Kitila Mkumbo anaongea na Clouds tv hasa katika kuchambua uongozi wa awamu hii katika nyanja kadhaa, anasema serikali imenuna na wananchi pia wamenuna sana
kiuchumi, mambo yalioyumba ni pamoja na Watumishi wa umma na wafanyabiashara
Aidha amesema serikali inapaswa kuongezea nguvu katika sekta binafsi kuliko kutegemea taasisi za serikali katika kutoa huduma mbalimbali, pia suala la elimu bado hakuna falsafa ya elimu nchini, kuhusu huduma za afya bado haijawa vizuri vilevile kwa mwaka mmoja uliopita 2016 katika siasa vyama vya siasa vilibanwa na dola,kulikua hakuna uhuru wa kujieleza, amelinganisha na awamu zilizopita zote zilizopita.Wakati wa Mh Mkapa kulikua na proper mixed economy na uchumi uliimarika
zaidi, lakini bado hajamuelewa Mh Rais Magufuli yupo katika dhana gani ya uchumi aitha anafuata wa Hayati Nyerere, Mwinyi ,Mkapa ama Kikwete

katika suala zima la uchumi
Wakati wa Rais Mkapa alifanya kazi nzuri katika kuboresha uwekezaji aitha kulikua na stability ya kisiasa na kuvutia wawekezaji

Chanzo: Clouds TV

Bado nasisitiza na kusema kuwa huyu Mtani wangu wa kutoka Mkoani Singida kwa aina ya IQ yake kubwa, nzuri na iliyotukuka leo hakupashwa kuzungukazunguka hovyo kama Inzi katika Vyama vya Siasa na badala yake angajikita sana katika Kukufunzi ( Lecturing ), Kufanya Tafiti ( Research ) na kutoa Ushauri wa Kitaalam ( Consultancy ) huko Chuo Kikuu alipo ili atuzalishie akina Mkumbos wengi ambao naamini wataweza kuibadili nchi hii na kuwa na msaada mkubwa nayo. Namkubali sana na mno Professor Kitila Mkumbo ila nisiwe Mnafiki wala nisifiche huko katika Medani za Siasa za Tanzania amepotea na si ajabu hata Credibility yake huko mbele ikashuka kutokana na aina za Siasa za Majitaka za Tanzania.
 
Mkataba wake wa kazi sijui ataongezewa na Mzee pale DUCE,acha aendelee kubwabwaja tu
 
Wataalamu na wasomi wetu kila siku in media watu wa kulalamika. Nguvu hizo wangewekeza kutoa majawabu. Sera kuu ni kukuza viwanda Taifa liwe nchi ya viwanda. Hicho ndio kipaumbele kikuu. Sasa ni kwa vip kinatekelezwa mjadala ungeanzia hapo... Je Macro Economics policy zinatekelezwa ipasasvyo ili kupata viwanda?
 
Back
Top Bottom