Kwa taarifa yako Prof. Baregu haamini kama kuna MUNGU. He is totally a pagan. Hii inasikitisha sana. MUNGU amsaidie ili atambue ya kuwa yuko MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake.
Le'njobe dhana ya Mungu na UUNGU , inatofauti sana , kwa jamii moja na nyingine, Ubora wa Mungu unategemea wewe unaabudu nini, ushenzi kwenye Imani unalalia kwenye dhana ya huyu si wetu, ama mwenzetu. ila kwa ujumla wake, Muhindu akiwatazama Waislamu ama Wakristo anaona viumbe dhalili, visivyomjua Mungu wa kweli, dhana hiyo anayo Muislamu dhidi ya dini za wengine vilevile Kwa Wakristo wao wanawaona wengine kuwa wanaabudu Miungu ilhali imeandikwa ...."mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu...."
sasa Ukiitazama Falsafa hiyo hakuna aliesahihi kumuhukumu mwenzake, maana hata yeye umzaniae amepotoka anakuona wewe , au sisi kuwa tuumepotoka kabisa.
kipo anachokiamini, lakini haamnini katika Mungu wa aina ya Waislamu, Wakristo ama Wahindu....?
Sio ajabu Baregu ni mlokole zaidi ya walokole wengine wanaojipigia debe, Mungu huangalia moyo wa mtu, hayumbishwi na mitazamo ya watu. Kama sivyo, Daudi asingepakwa mafuta kuwa Mfalme wa Israel mtoto mdogo asiyetarajiwa; Sauli (soma Paulo) asingekuwa mpiga debe maarufu wa Yesu Kristo hata kuwazidi mitume wengi waliotembea na Yesu miaka mitatu mfululizo. Mungu huwainua wangyone na kuwashusha wenye viburi. Nikodemus pamoja na kuwa msomi wa Kisamaria, alilazimika kutambua kwamba pamoja na kujulikana sana machoni pa watu kama mcha Mungu hakuwa na kitu, akalazimika kumwendeaYesu Usiku kula shule namna ya kuingia Mbinguni, Mungu akamkweza sana hata leo tunasoma habari zake. Yusufu ambaye hakutambuliwa na watu kama mwanafunzi wa Yesu akawa ndiye msaada wa kubeba msalaba wa Yesu kuelekea Golgotha wakati waliojulikana waliingia mitini.
Debe tupu mara zote haliachi kutika, Ngombale Mwiru amesemwa kwamba hana dini - ni makosa kusema hivyo, kwa sababu anayo dini ya mababu zake inayomtia nguvu kuwa mtu anayeishi na watu katika principles za imani ya dini yake. Neno zuri tuseme Baregu sio mkristo, hakuna dini ya kipagani. Waebrania waliwasema wasioamini kama wao "pagan", kama wachaga wanavyowaita "Kyasaka" wenzao na wanyakyusa wanavyowaita wenzao "Bhajanga", na wakinga huita "Bhanng'alu"..... Wapagani ni watu wasiokuwa na dini inayofanana na unayoiamini wewe. Kama ni kwa namna hiyo, basi tumtendee haki Baregu. Mbona ni mpole kupindukia na Mungu anapenda watu wapole? Ni mtu wa Mungu yule kama alivyo Mwislam, Mhindu, Myahudi, Mkristo, Budha na kadhalika.
Bwana Mazingira una haki kuamua kuelewa utakavyo, lakini bahati mbaya unavyonitaka nione kama ndivyo namaanisha sivyo. Sikia, dunia ipo tangu watu wawekwe na aliyewaweka. Watu huondoka lakini yenyewe dunia inaendelea kuwapo na wala wenye mawazo ya aina ako sio haba, usije ukajidanganya kwamba wewe ndie pioneer. Kingunge alikuwa anawaambia wasiotaka kufikiri kwa kina ili wakae walivyo. Ni vema ukitafuta kujua nini maana ya neno DINI, wala usimeze maneno kama unavyoyasikia. Dhana ya aina yako ndiyo JKN aliyowazodoa nayo waandishi wa habari wa Nairobi waliokuwa wanafikiria mambo juu juu kwa kuacha mambo aliyodhania yeye ni nyeti na wao hawakuona umuhimu. Waziwazi aliwaambia hawana akili kwa kuandika "Raisi Nyerer ampiga mkewe" badala ya kuandika mambo ya kimsingi yanayowasumbua watu ili kupata majibu yake. Aliwauliza kama Mr Kibuyu kule Musoma anampiga kila siku mkewe kwa jadi yao mbona hawaioni ni news ila Nyerere akimpiga mkewe kofi la mahaba tu inakuwa news ilhali naye anatoka jadi ileile ya Musoma.Hizi ndo zinaitwa hekima za watu wa dunia hii ambazo zimepoteza wengi. Unataka kutuambia kuwa kama babu yako alikuwa mwizi au jambazi na wewe ungependa kuwa kama yeye? Kisa cha mababu zetu kuabudu mizimu na mashetani na kuendekeza uchawi ndo unataka na sisi tuendelee kuabudu hayo? A big NO. Kingunge alishasema hana dini wewe unataka kumlazimisha awe na dini ya mababu zake kama nayo haitaki je? Si anao uhuru wa kuchagua atakacho mwenyewe?
wanalia timing afikishe sitini wamtoe nduki, na kama UDASSA Haitasimama kidete kweli elimu mlimani itaingia kaburini kabisa kabisa, maana bado ipo mahututi ICUI am happy for this BUT one question mbona Sengondo Mvungi ni mwanachama wa NCCR nauris aligombea na mara kwa mara amekuwa akitoa maoni kukosoa serikali lakini wanamwacha. Pia ni kwamba Tanzania kuna uhaba wa waadhiri kila nyanja mpaka wanaemploy foreigners kwa wingitoka India, Nigeria nk.