Privacy and security issues on WhatsApp

Mr Antidote

JF-Expert Member
Jan 11, 2015
952
1,293
Habari zenu wakuu!!
Leo ningependa kuwashirikisha baadhi ya vitu katika moja ya apps maarufu ya whatsApp ambavyo nadhani watu wengi hawafahamu.

Kama ni mtu ambae unajali usalama wa taarifa zako nadhani utakua umegundua kitu katika updates mpya ya whatsapp. Kifupi ni kwamba new updates ya sasa inakupa uwezo wa kujua kama mawasiliano yako na unae wasiliana nae yamefichwa (encrypted) au yako wazi (plain).

Namna gani utatambua mawasiliano yako na unaewasiliana nae ni siri?
1. Ingia katika account ya mtu unaemhitaji.
2. Nenda kwenye profile yake.
3. shuka chini kabisa kama unataka kusoma status yake.
4. Baada ya status utaona ujumbe una picha ya kufuli pembeni inayokuambia kama mawasiliano yenu yamefungwa au laah? Kama lugha itakua ni tatizo kuelewa basi angalia hiyo kufuli iko wazi au imefungwa. Kama imefungwa basi jua upo salama kwa kiasi fulani kwa hivyo ni ngumu mawasiliano yako kudukuliwa.

Nifanyaje kama bado mawasiliano yetu yapo wazi?
1. Awali ya yote ni ku-update whatsapp yako kama haipo up to date
2. Kama unaewasiliana nae haja-update basi muambie afanye hivyo kwa sababu bila ya wote kufanya hivyo hamtoweza ku-encrypty mawasiliano yenu.
3. Baada ya wote kufanya hivyo rudi tena kwenye profile ya muhusika kisha fuata hatua tatu za mwanzo za kujua kama mawasiliano yenu yapo encrypted then ukifika hapo tap(gusa) hapo kwenye ujumbe ambao utakupeleka moja kwa moja ku-verify encryption yako na hapo upo secure.

NB: Fanya hivyo kwa kila mtu ambae unachati nae sensitive information.

Kitu kingine ambacho ningependa kuwashilikisha ni kuhusu usiri katika utumaji wa picha na video.
Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja ambacho wengi nadhani hawakifahamu katika utumaji wa picha na video.
Utakuta mtu katuma picha au video kwa mtu halafu anataka asijulikane anachoamua kufuta ile video au picha au chati nzima kufuta ushaidi pasipo kujua kwamba ile picha bado ipo mule mule ndani ya simu yake ambapo kama mtu ana access ya simu yake anaweza kuziona.

Utajuaje kama bado ipo au umeifuta kabisa?
1. Nenda kwenye file manager ya simu yako
2. Ingia WhatsApp folder
3. Ingia kwenye media
4. Nenda kwenye image/video
5. Nenda mwisho kabisa wa video/images utaona file limeandikwa sent
6. Ingia kwenye hilo file la sent hapo utazikuta images/videos zako zote ambazo ulishazivuta katika chati zako.

Ili kuzifuta kabisa zifute tena humo na utakua umezifuta kabisa kwenye simu yako.

Hebu jenga picha kama simu yako iliharibika ukaipeleka kwa fundi akairekebishe na ulikua umemtumia mchepuko wako picha za "utam". Hii pia ni sababu kubwa ndio maana picha za utupu hazipungui mitandaoni.

Anyway kwa leo yanatosha bado nipo nachunguza kitu kingine nikikithibitisha nitawamegea tena.

Shukrani!!
 
Cha kuongezea actions zote unazofanya wasap zina seviwa ktk whatsapp folder la memory ya simu hata ku view picha ya mtu tu inakuwa saved ready hivo kama unataka privacy clear hilo folder frequently we are not safe 100℅
 
Hizi ndo madini zinatakiwa humu jamii forum sio kutwa kucha CCM na CHADEMA tu.
 
  • Thanks
Reactions: Ed5
Back
Top Bottom