President Kikwete to get fewer votes, says report | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

President Kikwete to get fewer votes, says report

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Mar 13, 2010.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Source: The Citizen.

  I do listening on these investigation or research.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Exuper Kachenje na Salim Said
  TAASISI ya Economist Intelligence United imetoa taarifa ya utafiti inayoonyesha kuwa kura atakazopata Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi wa mwaka huu zitapungua na kuonya kuwa iwapo rais ataendeleza vita dhidi ya ufisadi anaweza asiteuliwe na CCM kutetea urais.

  Kikwete, ambaye alipitishwa na CCM kugombea urais katika jaribio lake la pili baada ya kutoteuliwa mwaka 1995, aliibuka na ushindi mkubwa baada ya kuzoa kura 9,123,952 ambazo ni sawa na asilimia 80 ya kura zote, lakini tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbalimbali kama Synovate na Redet zimeonyesha kuwa umaarufu wa rais huyo unazidi kuporomoka.

  Na licha ya vyama vya upinzani kuonekana kujiepusha kupambana na waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, utafiti huo wa IEU unaonyesha kuwa kura kwa Rais Kikwete zitapungua kutokana na Watanzania kukatishwa tamaa na utendaji wa serikali yake.

  "Idadi ya kura atakazopata zinatarajiwa kuwa chini ya asilimia 80 ya kura ambazo alipata katika uchaguzi wa mwaka 2005. Hii inatokana na wananchi kukata tamaa," imeeleza taarifa ya utafiti huo yenye kurasa 24.

  Hata hivyo, utafiti umeeleza kuwa mbali na ushindi huo kiduchu, Rais Kikwete atabakia kuwa mtu maarufu kwenye utawala wake wa serikali ya awamu ya nne kama ripoti nyingine za utafiti wa Synovate na Redet zilivyoonyesha.

  "CCM bado inataka Rais Kikwete awe mgombea pekee wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kikwete anatarajiwa kushinda ingawa kwa idadi ndogo ya kura kutokana na wapiga kura kuonyesha kukata tamaa," inaeleza sehemu ya taarifa ya matokeo yab utafiti huo.

  "Kikwete ataendelea kuwa maarufu katika kipindi kilichobaki cha awamu yake ya kwanza ya uongozi, licha ya taifa kukabiliwa na mdororo wa kiuchumi, matukio makubwa ya ufisadi na kukua kwa mfumuko wa bei za bidhaa."

  Lakini taasisi hiyo yenye uzoefu wa miaka 60 katika masuala ya tafiti imeeleza kuwa pia kuna uwezekano wa Rais JK kutoteuliwa tena kugombea nafasi hiyo endapo ataendeleza vita ya ufisadi ambao watuhumiwa wengi ni wanachama wa CCM.

  "... kuna nafasi kidogo kwa Kikwete kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia CCM iwapo ataimarisha na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na kuwaburuza vigogo wa CCM mahakamani," inasema ripoti hiyo.

  Kwa mujibu wa taasisi hiyo vita ya ufisadi inaonekana kususiwa na wanasiasa na wasomi ndio maana hadi sasa hakuna hata mmoja aliyejidhihirisha kupambana na ufisadi na kama kutajitokeza mtu, atafanya hivyo baada ya uchaguzi mkuu.

  “Vita hiyo imesababisha mpasuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM,” inasema ripoti hiyo ya kwanza kuliangalia suala la ufisadi kwa kuhusisha na mustakabali wa mteule wa urais wa chama hicho tawala.

  Tangu mwaka 2006, vita ya ufisadi imekuwa ikifanywa ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano hasa baada ya kuibuka kwa sakata la utoaji zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC.

  Tayari mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu mmoja wamefikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao na kulisababishia taifa hasara,

  huku mlolongo wa wafanyabiashara na watumishi wa Benki Kuu (BoT) wakishtakiwa kwa tuhuma za kula njama na kuiibia benki hiyo mabilioni ya fedha zilizowekwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Hata hivyo, hadi sasa watuhumiwa wakuu kwenye wizi huo hawajafikishwa mahakamani huku wengine wakiepuka mkono wa sheria baada ya Rais Kikwete kutoa unafuu kwa kueleza kuwa wale ambao wangerejesha fedha hizo kabla ya Novemba mosi mwaka juzi, wasingeshtakiwa.

  Hata hivyo, ndani ya CCM vita hiyo inaonekana kuwa dhaifu kutokana na watuhumiwa wa ufisadi kuwa na nguvu zaidi.

  Vyombo vya habari viliripoti mwaka jana kuwa spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye amekuwa akionekana mmoja wa wapambanaji, alinusurika kutimuliwa kwenye chama akidaiwa kuruhusu mijadala inayokidhalilisha chama na serikali yake.

  Utafiti huo poia umebaini kuwa CCM na mwenyekiti wake Jakaya Kikwete wamekumbwa na homa ya uchaguzi, hali inayowafanya wahahe kila sehemu kuwashawishi wapigakura.

  “CCM imekumbwa na homa ya uchaguzi ndiyo sababu inayomfanya Kikwete kuhaha huku na kule kushawishi wapigakura kuwa yeye ndiye mgombea pekee atakayeweza kutatua kero zao na kukamilisha ahadi yake ya maisha bora (kwa kila Mtanzania),” EIU inasema katika taarifa hiyo.

  Katika kile kilichoelezwa kuwa mbinu ya kuendelea kujijengea umaarufu, ripoti hiyo imeeleza kuwa Rais Kikwete anaweza kupangua safu ya baraza la mawaziri kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, hatua hiyo itamsaidia kuweka sura mpya ya uongozi ambao atakuwa nao bega kwa bega hadi wakati wa uchaguzi.

  Taasisi hiyo imebainisha kuwa Rais Kikwete ameipa mgongo hofu ya wananchi kuwa uchumi wa nchi unayumba, huku akitumia muda mwingi kutafuta umaarufu wa kisiasa.

  Hata hivyo, utafiti huo unaonyesha kuwa Rais Kikwete na serikali yake wamekuwa wakijitahidi kuwajibika kuwekeza katika miundombinu, kuboresha uchumi mdogo kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa.

  EIU imemsifu Rais Kikwete binafsi kwamba ni kiongozi mwajibikaji kisiasa kwa viwango vya utawala wa Tanzania, ingawa serikali yake ina kiwango kidogo cha kujiamini kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Kuhusu vyama vya upinzani, EIU imesema kuwa ufanisi mdogo wa vyama hivyo utaisaidia serikali iliyo madarakani kupata mwanya wa kushinda kwa urahisi katika uchaguzi mkuu ujao na kutoa mfano wa kuanguka kwa vyama hivyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka uliopita.

  Lakini EIU imeweka bayana kuwa vyama vya upinzani vinaweza kupanga kususia uchaguzi mkuu, lakini kutokana na hali ilivyo havionekani kuwa vitaweza kutumia mbinu hiyo.

  Kuhusu kufikiwa kwa maridhiano ya Zanzibar, EIU imesema yatakuwa na ufanisi iwapo CCM itaweka mgombea anayekubali mabadiliko na kutokwamisha marekebisho ya katiba ya Zanzibar.
  Imetabiri kwamba machafuko yatatokea visiwani humo wakati wa uchaguzi mkuu, ingawa hayatafikia kiwango cha mwaka 2000 na 2005, ikiwa ulinzi hautaimarishwa.

  Kuhusu mtazamo wa uchumi wa Tanzania kisiasa, EIU imesema kwa mwaka wa 2010 uchumi utakua kwa asilimia 6 na kufikia asilimia 7 kwa mwaka 2011.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18493
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  REDET, Synovate, IEU, Shekhe Yahya na.......
   
 4. d

  damn JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Doe it means wizi wa kura utadhibitiwa mwaka huu ili asishinde kwa kishindo kama 2005?
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hii imekuwa namna mpya ya wasomi kula hela. Hivi kazi ya hawa wasomi wa mambo ya jamii ni kufanya survey tu ya jinsi uchaguzi utakavyofanyika? Ipo kazi. Wasomi wa nchi hii hawana msaada wowote wa maana. Nikutafuta namna ya kula na kupata umaarufu tu.
  Atleast Kenya kuna mama mmoja Prof amewahi kupewa tuzo la mazingira. Huku kwetu wana mazingira, wahandisi, madaktari na wanasiasa wote wanakuwa wana siasa.
   
Loading...