Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,318
- 7,982
- Thread starter
-
- #21
Jembe la power tiller ya mikono mifupi ni zito sana pawatila za mikono mirefu haziwezi kulivuta. Mashine huwa zinaelemewa sana na unaweza kusababisha matatizo mengine.Je majembe ya Power tiller ya mikono mifupi ambayo umeeleza kuwa ni mazito yanaweza yakafungwa kwenye Power tiller ya mikono mirefu na Power tiller ikafanya kazi kwa ufanisi uleule au itazidiwa na uzito wa jembe na kupunguza ufanisi?.
Je jembe kubwa kabisa ambalo linaweza kufungwa kwenye Power tiller ya mikono mirefu na power tiller ikaendelea kufanya kazi ya kulima kwa ufanisi uleule lina disc ngapi?.
planter za kupandia nafaka kwa kutumia Power tiller nazo zipo? na zinapatikana wapi na kwa kiasi gani?.
Powertiller inaweza kupiga heka ngapi kwa siku bila kusumbua?
Nasubiri majibu pia
Vipi kuna sehemu watu wanakodisha hizo power tiler ama mtu anaweza kupata used?Nimejibu tayari.
Nashukru, swali lingine nilikuwa nimeuliza hivi jembe la power tiller ya mikono mirefu ambalo linadisc nyingi ambalo power tiller ya mikono mirefu inaweza ikalivuta pasipo kuteteleka la mwisho kabisa linakuwa na disc ngapi? .Jembe la power tiller ya mikono mifupi ni zito sana pawatila za mikono mirefu haziwezi kulivuta. Mashine huwa zinaelemewa sana na unaweza kusababisha matatizo mengine.
Kinachofanyika watu huwa wanachukua disc za majembe mazito na kuzifunga kwenye majembe ya power tiller za mikono morefu. Hii huongeza ufanisi na kufanya kazi kwa uhakika kwani disc nzito huhimili visiki na maeneo magumu. Disc za mashine za mikono mirefu ni nyepesi ikikutana na kisiki au jiwe huwa zinapinda au kuchanika, vile vile huwa zinaisha faster.
Kuhusu planter za kuendeshwa na power tiller hizo sijaziona.
Used labda mitaani Kubota full umapata kwa 7-8 million. Kukodisha hapana, hazikodishwi labda kama utampata mtu mkaingia mkataba nae.Vipi kuna sehemu watu wanakodisha hizo power tiler ama mtu anaweza kupata used?
Power tiller inavuta jembe la disc mbili tu! Kuna vidisc mfumo wa harrow vipo vinne lakini havifai kwa matumizi yetu waafrica.Nashukru, swali lingine nilikuwa nimeuliza hivi jembe la power tiller ya mikono mirefu ambalo linadisc nyingi ambalo power tiller ya mikono mirefu inaweza ikalivuta pasipo kuteteleka la mwisho kabisa linakuwa na disc ngapi? .
je kwa upande wa trailer ni vipi?kwani kuna baadhi ya power tiller unakuta watumiaji wameondoa trailer original na kuweka za kuchongwa kienyeji wakati mwingine unakuta trailer hizo ni kubwa zaidi kupita zile ambazo power tiller inatoka nazo kiwandani na kuzifanya power tiller zibebe mzigo mwingi na mzito zaidi,hiyo haiwezi ikaiathiri Power tiller?.Power tiller inavuta jembe la disc mbili tu! Kuna vidisc mfumo wa harrow vipo vinne lakini havifai kwa matumizi yetu waafrica.
Ukichongea mwamba na kuongeza disc ziwe tatu nayo nzuri lakini utaongeza risk ya operator kuumia kwa kukatwa na kisu au kujigonga kwenye kisu. Idadi ya disc imezingatia usalama wa mwendeshaji wakati wa kazi.
Power tiller ambayo inaweza kuhimili kubeba mzigo wa trailer za kuchonga ni zile za mikono mifupi (16-20 HP). Ingawa watu wanafunga kwenye Power tiller za mikono mirefu.je kwa upande wa trailer ni vipi?kwani kuna baadhi ya power tiller unakuta watumiaji wameondoa trailer original na kuweka za kuchongwa kienyeji wakati mwingine unakuta trailer hizo ni kubwa zaidi kupita zile ambazo power tiller inatoka nazo kiwandani na kuzifanya power tiller zibebe mzigo mwingi na mzito zaidi,hiyo haiwezi ikaiathiri Power tiller?.
Kwa Power tiller za mikono mirefu ambayo ni nyepesi, kwa upande wa trailer la kutengeneza kienyeji trailer lake linatakiwa liwe na upana wa ft ngapi ili power tiller isiweze kuathirika?.
Lengo likiwa ni nini? Jibu ni ndio unaweza kubadili tairi lakini utatakiwa kuchongea matundu mengine maana matundu ya stadi za kubota hayaingiliani.Mkuu mimi nina powertiller ya mikono mifupa naomba ushauri, je naweza kubadilisha tairi ndogo na kuweka za siam kubota upande wa injini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Je power tiller inaponunuliwa inakuja na water pump au water pump inanunuliwa kivyake?.Lengo likiwa ni nini? Jibu ni ndio unaweza kubadili tairi lakini utatakiwa kuchongea matundu mengine maana matundu ya stadi za kubota hayaingiliani.
Kama lengo ni kuongeza speed basi weka puli ya mashine za kusaga za diesel na pawatila itakimbia kama kubota bila kubadili tairi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Puli nmeshabadilisha nataka kuongeza spidi na kusave mafuta, kingine injini ya powertila mikono mifupi ni nzito na inamaliza tairi mapema so nikiweka zile za kubota nahisi hazitaisha mapema.Lengo likiwa ni nini? Jibu ni ndio unaweza kubadili tairi lakini utatakiwa kuchongea matundu mengine maana matundu ya stadi za kubota hayaingiliani.
Kama lengo ni kuongeza speed basi weka puli ya mashine za kusaga za diesel na pawatila itakimbia kama kubota bila kubadili tairi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Min tractor zinakufa haraka sana sijui ni mazingira ya huku kwetu! Ngoja niwaulize wanaozimiliki nitakupa mrejesho.Mkuu naomba pia kujua kuhusu Mintractors kama itawezekana
Ni tiller gani inafaa kwenye kupalilia Mkonge?Wale wanaohitaji kuzielewa power tiller karibuni.
Uzi huu utatumika kujibu maswali na majibu ya wadau ambao wamekua wakiniuliza mara kwa mara.
Kuna aina kuu mbili za power tiller yaani Long hand power tiller na Short hand power tiller.
LONG HAND POWER TILLER
Long hand power tiller ni zile zenye mikono mirefu ya kuendeshea kama ville Siam Kubota, Boar, Toyo, Myanmar(hazipo nchini), Swami, N.k
Power tiller hizi zote huwa ni 14 HP, 4 gear na magurudumu ya mbele makubwa kiasi. Powetiller hutoka ikiwa na cage wheel, disc plough na leki kwaajiri ya kupigia level na kuokota.
Bei zake nchini ni million 5 au pungufu kwa aina nyingine zote( India and chinese) bila tera na 7.5 million ikiwa complete. Hazidumu sana kwani huanza kusumbua gear box na engine ndani ya mwaka mmoja au miwili toka kununuliwa. Zinadumu kwa miaka 7 - 10 zikitunzwa vizuri.
Zinafaa kwenye kilimo cha mahindi na kilimo kingine kinachofanana na hicho.
Bei ni 9.5- 10 Million kwa Siam Kubota (Japan) bila tera na 12-14 million complete. Hudumu kwa muda mrefu up to 15 years na inaweza kufanya kazi miaka 3 bila serious service ya engine wala gear box. Shida ya hizi mashine ni ghalama kubwa zaa spea.
Hizi hukimbia sana na hufanya kazi kwa uharaka zaidi. Vile vile ni nyepesi kuopoa kama zikikwama kwenye tope wakati wa kuvuruga. Zinafaa kwa matumizi yoyote ya kilimo na katika mazingira yoyoye isipokuwa Yale yenye visiki kwani jembe lake si imara sana.
Picha hizi hapa.
View attachment 1275195View attachment 1275196View attachment 1275197View attachment 1275201View attachment 1275202
SHORT HAND POWER TILLER
Short hand power tiller ni zile zenye mikono mifupi ya kuendeshea kama vile Amec, Kubota(ndogo), Toyo, Greeves, Jiang Dong (JD), Zhong Hou (ZH) n.k.
Power tiller hizi huwa na 13 HP mpaka 20 HP kutegemeana na uhitaji wa mteja. Bei zake huanzia million 3.5 bila tera mpaka million 7 ikiwa full.
Power tiller hizi hutoka ikiwa na disc plough,Rotavator na cage wheel za kwenye maji.
Machine hizi huwa na gia 8 na hazikimbii sana lakini zinanguvu kubwa. Zinafaa kwenye kilimo cha aina yoyote. Tatizo kubwa la hizi machine ni kufa haraka yaani hazikai zaidi ya miaka 7 kama zinafanya kazi kweli kweli.
picha hapa chini
View attachment 1275204View attachment 1275205
MASOKO
power tiller hizi zinapatikana nchini sehemu Mbali mbali kama vile
Iringa - Auto sokoni ( aina zote), Kishen Inter prices( Toyo tu) na maduka mengine ya spear na power tiller
Dar es salaam - kishen pia wapo, na ofisi nyingine sizijui( watanisaidia wenyeji).
Agricom wanaopatikana morogoro na Mbeya na mikoa mingine.
Kwa Mbeya zinapatikana sehemu kubwa zenye kilimo cha mpunga.
Mikoa mingine zipo kwenye maduka mbali mbali ambayo yanapatikana huko.
Kama unauza utanitajia jina na mkoa ili nipandishe hapa.
Karibuni kwa maswali, maoni na nyongeza.