jamaa (Membe) alikuwa akitoa taarifa kwa majivuno na majigambo yaani!! , ana 'confidence' kweli kututaarifu umma kuwa wapo kwenye mchakato mwingine wa kuwawezesha wanafunzi kupata madawati, waalimu kujengewa nyumba na tantalila miiingi kama ilivyo ada kusema ni rahisi, suala ni utekelezaji... halafu mi najiuliza .....kama hizi pesa imedhihirika ziliibwa, sasa mbona sikumsikia akiwaongelea waliohusika na wizi huo?!! maana wanajulikana!! huyo dalali kanjibahi mla pilipili si anajulikana?! waliohusika na manunuzi si wanajulikana?!!
halafu it is known kuwa wizi wa pesa za mtanzania upo kwenye malipo na manunuzi....bado tena wanatengeneza namna za kufanya manunuzi na malipo kwa pesa zilizoibiwa kutokana na malipo ya manunuzi !!! JAAAAAAH!!! tuombe uzima, am telling you wanajamii hili litazungumzwa, litapita... madawati hayataonekana kama yatanunuliwa lazima watu watakula chao, dawati 1 la wnafunzi wawili utasikia laki 3 au nne, wakati likizidi sana elfu 90 au laki moja.... hizo nyumba nazo zitaundiwa "tume ya uratibu wa mchakato wa upangaji mkakati kufanikisha utekelezaji" (wizi mwingine in the making).