Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,315
Kubali Matokeo!
Ilikuwa mapema sana asubuhi, mitaa ikiwa safi na isiyo na watu, nilikuwa nikitembea kwenda stesheni. Wakati nikilinganisha muda unaosemwa na saa ya kwenye Mnara wa Saa na ile niliyoivaa mkononi, nilitambua kwamba muda ulikuwa umeenda sana kuliko nilivyodhani, ikanibidi kuharakisha, mstuko wa utambuzi ulinifanya niwe na mashaka ya njia ni ipi, sikuujua mji huu vizuri; kwa bahati, polisi mmoja alikuwa karibu, nikamkimbilia, huku nikihema nikamuuliza njia. Alitabasamu na kusema: "Unataka kujua njia kwa kuniuliza mimi?"
"Ndio," nilijibu, "kwa vile mimi mwenyewe siijui"
"Kubali matokeo! Kubali matokeo," alisema, na kugeuka nyuma ghafla, kama wafanyavyo watu wanaotaka kujificha wachekapo.
MWISHO
Edit1: Change from Potezea to Kubali Matokeo
Hadithi hii iliandikwaga na Franz Kafka mnamo takriban mwaka 1917 kwa Kijeremani ikiitwa Gib's Auf!.
en.wikisource.org