Posts nyingi za kipuuzi za vijana wa Tanzania hasa Twitter zinaeleza tuna kizazi cha namna gani

Twitter ukweli siku hizi imekuwa na vijana wa hovyo hovyo sana sijui ni malezi gani haya hawa vijana wamelelewa
Nimekuwa naingia mara chache sana kulinganisha na miaka ya 2010/12/13.
Twitter wamejaa graduates wengi ambao ni majobless wanatafuta followers wengi ili wapewe kazi za kupush hashtags kama mainfluecers...ndio wanaandika upuuzi ili kupata followers si unajua wabongo akili zao zinapenda kusikia masuala ya ngono..pesa..starehe na pombe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sijui ni kwangu tuu, kipindi cha nyuma app ya twitter ilikuwa inaniletea posts za watu ambao nimewa'follow ila sasa hivi kuanzia yule niliyem'follow na baadhi ya ambao kawafollow yeye posts zao naziona kwa wingi sana. Sijui hata kwanini nili update App.
 
Kushindikana kwa malezi miongoni mwa wazazi wa kileo kuna reflect katika maudhui hasa ya vijana wanaoyumkinika kuwa wasomi kwenye mtandao pendwa wa twitter.

Nimeichagua Twitter kwa sababu imejipambanua kuwa host vijana wengi wasomi.

Ukifuatilia mada wanazopakia kufollow na kulike unagundua kwamba hata wasomi tunaozalisha uwezo wao wa kumudu mazingira umeishia kushabikia upuuzi wa ngono, pombe na anasa za kupindukia.

Katika hali hii wajanja wachache ni rahisi sana kutoboa sababu tuna kundi kubwa la vijana 'wasomi' ambao wanaendekeza upuuzi.

Jamii zetu zina changamoto sana ilifaa social media vijana waitumie kusocialise kwa staha na kusaidia kutatua changamoto za jamii na zinazowakabili ila sasa ni ngono ngono ngono ngono...pombe pombe pombe...

No wonder wageni wakiwemo Wakenya wanavuna sana hapa nchini maana washawasoma wabongo vijana kupitia social media kwamba hawa hamnazo.

Ukipost kilimo unatukanwa...ukipost ujasiriamali unanangwa...ukipost viungo vya kukalia vya wamama unapongezwa unakuwa followed na posts zako zinapata majority likes...sisi ni bure sana...wakenya njooni mvune si tupo kulana kimasikhara
Kwakuwa umeamka ukijitoa huko wapuuzi watapungua
 
Twitter bado kuna vijana wapo vizuri Tu mkuu ambao ukiconnect nao wapo vizuri Ila kwa kiasi kikubwa ulichoongea ni kweli mkuu

Wengi wanatukana na kudhalilisha watu, kupost upuuzi ili wapate likes na retweets na mbaya zaidi imeshaanza kuwa desturi,

Cha msingi ni kufollow na kuchanhgamana na watu unaowataka, mengine unaachana nayo Tu mkuu
 
Na mwaka sasa nmeondoka TWITTER kumevamiwa na wapuuzi sana..tunawaita vijana wa hovyo..

#MaendeleoHayanaChama
Twitter ni nzuri sana ni wewe tu uchague page za maana,mfano, mimi nimewa follow kina Ay,Salama jabbir na viongozi kadhaa huko congo pamoja na pages za mambo ya ujenzi wa makazi
 
Ukipost kilimo unatukanwa...ukipost ujasiriamali unanangwa...ukipost viungo vya kukalia vya wamama unapongezwa unakuwa followed na posts zako zinapata majority likes...sisi ni bure sana...wakenya njooni mvune si tupo kulana kimasikhara

🤣🤣🤣🤣
 
Nadhani ni Mda wa kuanza kuleta Solution Ya namna ya kutatua changamoto hii, Ambayo inaoneka kwa Sasa ni tatizo kubwa, ili tuweze kuwa na Taifa lenye mawazo ya kujenga zaidi kuliko kushinda mitandaoni siku nzima bila ya kuingiza kitu cha maana.
 
Shida moja watu ni ndumilakuwili, kwenye post hii watakuunga mkono utasema kwenye zile post zingine hawapo, kumbe nako ndio wanaongoza kutuma madude yao
 
Ukienda na content Za ufugaji au kilimo huwezi kupata followers kule, wewe weka chachandu n.k ndio maana kuna parody nyingi kule,
 
&g&
Na mwaka sasa nmeondoka TWITTER kumevamiwa na wapuuzi sana..tunawaita vijana wa hovyo..

#MaendeleoHayanaChama
Inategemea na watu au page ulizo follow na post unazolike, ukiwa una like post za kijinga zile algorithm zao wanakuletea post za kijinga kwenye wall yako
 
Platform ya kupaza saut, ku brainstorm ideas kushea vumbuzi wanatumia kufanya ung'ombe na kadri maudhui yanavyokua ya kipimbi ndio kadri fanani anavyozid kupendwa, hilo ni tatizo
Ndio muwape ajira wajishughulishe wachangamshe akili wanasema idle mind ni makazi ya shetani
 
Lack of exposure tu hiyo mnaishia ku follow watu wanao wazunguka ndani ya nchi mnaishia kusema WaTz ina vijana wa hovyo... Embu mjaribu kufuatilia contents za watu au vijana wa nchi nyingine za Africa Asia Europe and America... Wanapost ujinga mwingi sana tena afadhali ya WaTz tuna jitahid kulinda maadili... All in all hii mitandao ya kijamii tusiichukulie serious sana no sehém ya watu ku-enjoy, kwahio msihukumu watu... Sasa wewe mhukumu mtu kwasabab ktk mitandao anaish vile basi ukamletea maisha hayo ktk maisha yake nje ya mitandao uone atakavyo kushangaa na upuuzi wako...
Asante mkuu.

Watu wanashindwa kutofautisha maisha ya mtandaoni na uhalisia..

Tena kule unaweza kukuta sio vijana tu hadi watu wazima na wanao jiheahimu ndio wanafanyia uupuuzi kule nyuma ya pazia ni watu smart sana.

Kila mtu atafute kile anapenda
 
Back
Top Bottom