Pongezi kwa Real Madrid kuchukua UEFA ya 12,kweli niliwakosea sana heshima

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
2262058_w2.jpg

FAINALI YA UEFA 2017 WANAUME DHIDI YA WANAUME
Five-todos-for-Cristiano-Ronaldo-in-the-UEFA-Champions-League-696x464.jpg

Christiano Ronaldo amethibitisha kuwa yuko peke yake kwenye hii dunia.
upload_2017-6-4_21-30-5.png

Hakuna Ronaldo mwingine,kwenye Fainali ya jana ilikuwa bonge la fainali.Mpira ulianza kwa kasi huku juventus wakitafuta goli la mapema.madrid walitulia nyuma huku juventus wakijaribu kusaka goli la mapema japo hawakufanikiwa.Baada ya dakika 15 za kwanza za mchezo Juventus walipunguza kasi ya kushambulia jambo lililowapa Madrid walau nafasi ya kujaribu kufika kwenye lango la juventus..Hapa ndipo picha halisi ya mechi ilianza kuonekana..
upload_2017-6-4_21-32-27.png

Juventus walishambulia na Madrid wakashambulia kiasi lakini Madrid walipata nafasi ambayo Ronaldo alimchungulia kipa Buffon na kuweka mpira kambani..

Juventusi walijitahidi kushambulia huku Madrid wakijaribu kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza lakini juventus walipata nafasi ambapo Mario mandzukic alifunga goli zuri kabisa na baada ya hapo juventus walirudi nyuma na kuzuia huku Madrid wakishambulia mpaka refa alipo puliza kipyenga cha mwisho(half time)..

Kipindi cha pili juventus walianza kwa kujilinda zaidi hali iliyoifanya Real Madrid kushambulia kwa kasi..juventus walikuwa wakingojea kushambulia kwa kushtukiza..hali hii ya kujilinda kwa juventus ili sababisha Madrid kusakama lango la juventus lakini mabeki na viungo wa juventus walijilinda vizuri halio iliyo fanya ronaldo na benzema kukosa mipira kutoka kwa modric,isco na kroos...

Real Madrid walipata goli ambalo casemiro alipiga shuti kali nje ya box lililo mpita kipa buffon.goli hilo liliwafanya Juventus kusogea mbele kushambulia kwa kasi hali iliyo wafanya benzema na ronaldo kuweza kupata nafasi ya kucheza kwenye final third ya real Madrid.

Hata hivyo mabadiliko ya juventus ya kuongeza ushambuliaji haya kuweza kuzaa matunda kwakuwa walikuwa wamezuiwa vizuri na Madrid kiasi kwamba hata Dyabala kukosa nafasi muda wote wa mchezo.Dybala alifichwa kabisa kwenye mchezo wa jana kiasi kwamba mpaka ikabidi atolewe kipindi cha pili. Juventus walikuja na mbinu ya kushambulia kwa kasi na kukaba kwa kasi hali iliowafanya Madrid kushindwa kumiliki mpira.Wali tengeneza mashambulizi makali huku wakiwatumia sana Dani Alves na Alex sandro kwa kuleta mipira ya krosi kwa mandzukic na higuain..

Alves na Sandro walipanda kwa kasi na walizuia kwa kasi huku pjanic na khedira wakisogea katika boksi la madridi kungojea mipuira ambayo angeokolewa na mabeki wa Madrid kutokana na krosi za alves na sandro..dybala alikuwa akiingia ndani ya boksi kuongeza idadi ya washambuliaji katika box la madrid hali iliyowapa ugumu mabeki na viungo wa real Madrid kuweza kuwazuia juventus kipindi cha kwanza. Zidane alikuja na mbinu ya kuwa na midfielders wanne..casemiro,isco,modric na kroos.isco alicheza zaidi upande wa kushoto ambapo alikuwa na jukumu la kumzuia Dani alves..

Hivyo kazi haikuwa ngumu sana kwa Marcelo kuweza kumzuia dani alves.luka modric alicheza zaidi upande wa kulia ambapo aliweza kumzuia vizuri alex sandro aliye kuwa na speed kali..

Carvajaal alitakiwa kuweza kuwa free ili kuweza kumzuia mandzukic. kadi ya njano aliyo ipata carvajaal ilitokana na kumkaba na kumchezea rafu mandzukic.to tini kroos na Marcelo walikuwa na kazi ya kuwazuia dybala na pjanic wanapoingia ndani ya box. Madrid walipo kuwa wakishambulia Marcelo na Carvajaal walikuwa wakikimbia kwa speed pembeni (kulia na kushoto) huku modric na isco wakiingia ndani ambapo casemiro alikuwa akibaki eneo la kati na kroos alikuwa akisogea mbele zaidi hali iliyo wapa kazi ngumu pjanic na khedira wakati huo ronaldo na benzema walikuwa wakiwasumbua sana mabeki wa kati wa real Madrid..ronaldo alikuwa mjanja zaidi hali iliyopelekea kuwazidi maarifa mabeki wa kati watatu wa juventus na kufunga magoli mazuri mawili.Modric na Isco walikaba na kumiliki mpira vizuri mno hali iliyo wafanya benzema na ronaldo kuweza kujipanga vizuri na kuwasumbua juventus.Ronaldo alikuwa katika kiwango bora zaidi japo kuna muda alikuwa amefichwa kabisa.

Mabeki wa kati wa Madrid walikuwa wana masiliano mazuri kati yao na goli kipa kitu kilicho wafanya kutokuweza kufanya makosa wakati wa kuokoa..

Ila hatimaye mambo yakawa hivi pale Cardiff

Real-Madrid-Juara-Final-UCL-2017.jpg

Pongezi kwa real Madrid kwa taji la 12 la UEFA ,pia zidane kwa taji la pili mfulizo kama kocha ,ronaldo kwa tuzo ya tano mfululizo ya top goal scorer wa champions league na wachezaji wote wa Madrid kwa kuandika historia hii kubwa katika UEFA.

Pongezi pia Juventus kwa kufika fainali na kufanya game ya fainali kuwa kali kabisa.
 
2262058_w2.jpg

FAINALI YA UEFA 2017 WANAUME DHIDI YA WANAUME
Five-todos-for-Cristiano-Ronaldo-in-the-UEFA-Champions-League-696x464.jpg

Christiano Ronaldo amethibitisha kuwa yuko peke yake kwenye hii dunia.
View attachment 519336
Hakuna Ronaldo mwingine,kwenye Fainali ya jana ilikuwa bonge la fainali.Mpira ulianza kwa kasi huku juventus wakitafuta goli la mapema.madrid walitulia nyuma huku juventus wakijaribu kusaka goli la mapema japo hawakufanikiwa.Baada ya dakika 15 za kwanza za mchezo Juventus walipunguza kasi ya kushambulia jambo lililowapa Madrid walau nafasi ya kujaribu kufika kwenye lango la juventus..Hapa ndipo picha halisi ya mechi ilianza kuonekana..
View attachment 519338

Juventus walishambulia na Madrid wakashambulia kiasi lakini Madrid walipata nafasi ambayo Ronaldo alimchungulia kipa Buffon na kuweka mpira kambani..

Juventusi walijitahidi kushambulia huku Madrid wakijaribu kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza lakini juventus walipata nafasi ambapo Mario mandzukic alifunga goli zuri kabisa na baada ya hapo juventus walirudi nyuma na kuzuia huku Madrid wakishambulia mpaka refa alipo puliza kipyenga cha mwisho(half time)..

Kipindi cha pili juventus walianza kwa kujilinda zaidi hali iliyoifanya Real Madrid kushambulia kwa kasi..juventus walikuwa wakingojea kushambulia kwa kushtukiza..hali hii ya kujilinda kwa juventus ili sababisha Madrid kusakama lango la juventus lakini mabeki na viungo wa juventus walijilinda vizuri halio iliyo fanya ronaldo na benzema kukosa mipira kutoka kwa modric,isco na kroos...

Real Madrid walipata goli ambalo casemiro alipiga shuti kali nje ya box lililo mpita kipa buffon.goli hilo liliwafanya Juventus kusogea mbele kushambulia kwa kasi hali iliyo wafanya benzema na ronaldo kuweza kupata nafasi ya kucheza kwenye final third ya real Madrid.

Hata hivyo mabadiliko ya juventus ya kuongeza ushambuliaji haya kuweza kuzaa matunda kwakuwa walikuwa wamezuiwa vizuri na Madrid kiasi kwamba hata Dyabala kukosa nafasi muda wote wa mchezo.Dybala alifichwa kabisa kwenye mchezo wa jana kiasi kwamba mpaka ikabidi atolewe kipindi cha pili. Juventus walikuja na mbinu ya kushambulia kwa kasi na kukaba kwa kasi hali iliowafanya Madrid kushindwa kumiliki mpira.Wali tengeneza mashambulizi makali huku wakiwatumia sana Dani Alves na Alex sandro kwa kuleta mipira ya krosi kwa mandzukic na higuain..

Alves na Sandro walipanda kwa kasi na walizuia kwa kasi huku pjanic na khedira wakisogea katika boksi la madridi kungojea mipuira ambayo angeokolewa na mabeki wa Madrid kutokana na krosi za alves na sandro..dybala alikuwa akiingia ndani ya boksi kuongeza idadi ya washambuliaji katika box la madrid hali iliyowapa ugumu mabeki na viungo wa real Madrid kuweza kuwazuia juventus kipindi cha kwanza. Zidane alikuja na mbinu ya kuwa na midfielders wanne..casemiro,isco,modric na kroos.isco alicheza zaidi upande wa kushoto ambapo alikuwa na jukumu la kumzuia Dani alves..

Hivyo kazi haikuwa ngumu sana kwa Marcelo kuweza kumzuia dani alves.luka modric alicheza zaidi upande wa kulia ambapo aliweza kumzuia vizuri alex sandro aliye kuwa na speed kali..

Carvajaal alitakiwa kuweza kuwa free ili kuweza kumzuia mandzukic. kadi ya njano aliyo ipata carvajaal ilitokana na kumkaba na kumchezea rafu mandzukic.to tini kroos na Marcelo walikuwa na kazi ya kuwazuia dybala na pjanic wanapoingia ndani ya box. Madrid walipo kuwa wakishambulia Marcelo na Carvajaal walikuwa wakikimbia kwa speed pembeni (kulia na kushoto) huku modric na isco wakiingia ndani ambapo casemiro alikuwa akibaki eneo la kati na kroos alikuwa akisogea mbele zaidi hali iliyo wapa kazi ngumu pjanic na khedira wakati huo ronaldo na benzema walikuwa wakiwasumbua sana mabeki wa kati wa real Madrid..ronaldo alikuwa mjanja zaidi hali iliyopelekea kuwazidi maarifa mabeki wa kati watatu wa juventus na kufunga magoli mazuri mawili.Modric na Isco walikaba na kumiliki mpira vizuri mno hali iliyo wafanya benzema na ronaldo kuweza kujipanga vizuri na kuwasumbua juventus.Ronaldo alikuwa katika kiwango bora zaidi japo kuna muda alikuwa amefichwa kabisa.

Mabeki wa kati wa Madrid walikuwa wana masiliano mazuri kati yao na goli kipa kitu kilicho wafanya kutokuweza kufanya makosa wakati wa kuokoa..

Ila hatimaye mambo yakawa hivi pale Cardiff

Real-Madrid-Juara-Final-UCL-2017.jpg

Pongezi kwa real Madrid kwa taji la 12 la UEFA ,pia zidane kwa taji la pili mfulizo kama kocha ,ronaldo kwa tuzo ya tano mfululizo ya top goal scorer wa champions league na wachezaji wote wa Madrid kwa kuandika historia hii kubwa katika UEFA.

Pongezi pia Juventus kwa kufika fainali na kufanya game ya fainali kuwa kali kabisa.
Good! You have analyse well man!
 
Back
Top Bottom