Polisi yazuia kongamano la vijana mkoani Simiyu, je kuna haja ya kuwa na siasa?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Ndio sababu zitolewazo
30d29fe8-1eb2-4078-b26d-dcf1e22e55c2.jpg
7a2920bb-eaa0-47fe-ab13-eccd36d6c53e.jpg
 
Polisi hawana akili sasa mbunge wa vitu maalumu mwanasiasa akiitisha mkutano utakuwa wa kusoma bibilia au kisiasa wanachokipalilia polisi hawataweza kukidhibiti kwanza njaa tupu hawana uwezo hata wa kufikiri
Hayo mambo ya kisiasa yenye sura ya namna hiyo yalikatazwa hadi yatakapotolewa maelekezo mengine.Elekezeni nguvu kwenye maswala yanayowagusa wananchi kv kuhakikisha kua madawati ya kutosha yanapatikana katika majimbo yenu ili watoto wetu waache kukaa chini wakati wa kusoma,mda wa siasa umekwisha hadi 2020
 
Angekuwa na ka akili kidogo tu cha kufahamu nini maana ya siasa pengine uzi huu usingekuwepo au usingekuwa kama ulivyo hapa. Hauna maana yoyote, haufundishi chochote, haufikirishi wala hauibui mawazo mapya isipokuwa tu kufikirisha uwezo na akili za mtu aliyeuleta
 
Ninavyojua makongamano huandaliwa na taasisi zilizosajiliwa sio mtu kujiibukia tu eti nimeandaa kongamano!!!!

Huu kwanza si wakati wa makongamano pelekeni madawati Simiyu huko AU VITABU
 
Rais keshasema....sasa uchaguz umeisha mambo ya siasa siasa wasubir baada ya miaka mitano....Hapa kazi tu
 
Nchi hii ni yetu sote na siyo ya jeshi la polisi na serikali yake, suala la kuzuia kongamano la vijana katika kupeana uelewa juu ya fursa za kiuchumi si haki, kwani wanarudisha nyuma juhudi za vijana katika kujikwamua na lindi la umaskini wakati serikali iliyopo madarakani inataka vijana kufanya kazi, sasa kama wanazuiwa kupeana uwezo katika kujitafutia kipato hakika ni shida kubwa ambayo haivumiliki
 
Back
Top Bottom