kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
WATU wanne wanaotuhumiwa kuwa majambazi wameuawa na Polisi mkoani hapa walipokuwa wakifanya jaribio la kutoroka mikononi mwa polisi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zelothe Stephen alisema jana kuwa watuhumiwa hao walijeruhiwa juzi saa tano usiku katika mtaa wa Chinyele Kata ya Nzuguni nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma na walikufa walipokuwa wakikimbizwa hospitalini.
Kamanda Zelothe alisema watuhumiwa hao wapatao sita wakiwa na silaha mbalimbali zikiwemo za kivita aina ya SMG na shotgun, walivamia duka la mfanyabiashara ambaye jina lake limehifadhiwa na kupora kiasi cha Sh laki tano na bidhaa mbalimbali zikiwemo simu tatu za mkononi.
Alifafanua kuwa uporaji huo ulifanyika mara baada ya majambazi kufyatua risasi kadhaa katika eneo hilo na kumjeruhi mfanyabiashara huyo kwa chupa ya bia kichwani.
Wakati polisi wakiwasili eneo la tukio, walikuta majambazi yalishatoweka katika eneo hilo ambapo waliokota maganda mawili ya risasi zilizotumika na risasi moja ambayo ilikuwa haijatumika.
Kamanda Zelothe alisema Polisi ilipata taarifa za siri zilizotolewa usiku huo na kuanzisha msako mkali uliofanikisha kuwapata watuhumiwa hao wakiwa wamejificha katika nyumba moja eneo la Changombe Manispaa ya Dodoma.
Alisema kati ya watuhumiwa hao, alikamatwa mtuhumiwa mmoja wa ujambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Shedrack William ambaye ni mkazi wa Mpama katika Manispaa ya Dodoma.
Kamanda Zelothe alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa muda mrefu kwa tuhuma za ujambazi uliofanyika mwaka jana eneo la Fufu wilayani Chamwino.
Nyumba ambayo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wamejificha ilipekuliwa ambapo bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba 56-396-6946 na magazini moja ndani yake ikiwa na risasi tatu ilikamatwa.
Pia polisi ilikamata baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuwa ziliporwa dukani kwa mfanyabiashara huyo wakati wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda Zelothe, wakati polisi wakihojiana na watuhumiwa hao walikubali kuwapeleka polisi sehemu ambapo silaha nyingine ilikuwa imefichwa katika eneo la Nzuguni jirani na sehemu inayodaiwa kuwa uhalifu huo ulifanyika.
Alisema kwenye eneo hilo jirani na shamba la mahindi, watuhumiwa hao walionesha silaha aina ya shotgun iliyokuwa imekatwa mtutu na kitako na kufutwa namba zake.
Mbali na silaha hiyo, zilipatikana risasi 17 za bunduki hiyo na risasi 68 za SMG ambavyo vilikuwa vimefungwa kwenye mfuko wa sandarusi.
Wakati polisi wakipekua eneo hilo kwa makini, watuhumiwa hao wa ujambazi wanadaiwa walijifanya wanataka kukaa chini na kisha wakajaribu kukimbia katika shamba la mahindi kuelekea maeneo tofauti, hali iliyowafanya askari kufyatua risasi hewani.
Kamanda Zelothe alisema wakati askari wakiendelea kufyatua risasi hewani, watuhumiwa hao walizidi kutokomea ndipo walipolazimika kuwajeruhi ili kuwatia nguvuni na kuwakimbiza hospitalini ambapo daktari alithibitisha kuwa tayari walikwishakufa.
Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa utambuzi na taratibu nyingine za kisheria.
Polisi imetoa mwito kwa wananchi mkoani hapa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo
Kwa kutumia common sense, inakuwaje unamkamata mtuhumiwa wa ujambazi unamuacha akitembea free, si hata wangefunga kamba? Lingine linaloshangaza, hivi hawa polisi wetu wanafundishwa kuua au kukamata. Kama kungekuwa na majibizano ningeelewa, maana hiyo ni vita. Watu wanne wanaokimbia, wote wanapata majeraha ya kusababisha vifo? Kuna jambo linalofichwa hapa.
kwani polisi wanatakiwa kuwapiga risasi sehemu gani wahalifu wanaojaribu kutoroka?
polisi wetu wa tz wa std 7/form 4, hawafundishiki!kwani polisi wanatakiwa kuwapiga risasi sehemu gani wahalifu wanaojaribu kutoroka?
Wawaulize wenzao Uganda, hawana kazi sababu ya vitambiAskari wetu hawana mazoezi na mbinu za kukabiliana na wahalifu. wao wnachoweza ni kutumia silaha tu.
Hii inatisha kweli. Hao polisi wanatakiwa wafikishwe mahakamani lazima wana kesi za kujibu, uzembe, kutokua makini kazini na kusababisha vifo. Habari yenyewe ilivyokaa ni ya kutunga. hii ni Zombe stail.
Staili ileile ya akina Zombe. Lakini whats is new here?
Mkuu hv rufaa ya kina zombe imeishia wapi?Staili ileile ya akina Zombe. Lakini whats is new here?
This is no longer news. Same story, copy and paste kinachobadilishwa ni mkoa, rpc na idadi ya majambazi. Ukisoma between lines haileti sense hata kidogo
1. Majambazi wanne kwenda kuonesha silaha moja, was it necessary.
2. Kama tayari walikuwa na silaha kwa nini polisi walienda kichwa kichwa
porini kuoneshwa silaha, waliwaamini vipi hao. Polisi hawakuwa wanaweka
maisha yao at risk.
3. Kwa nini majambazi wasifungwe pingu, au polisi wanasubiri matokeo ya
tume ya pingu za Muro?
4. Walilazimika kuwajeruhu kwa namna gani na polisi walikuwa wangapi
kwenye operesheni hiyo.
Waandishi wa Dodoma mnaweza kufuatilia leads hizo, mtapata story kabambe i swear. Achaneni na press statement za polisi ni kutunga.
Mara nyingi sana Police huwa lengo lao siyo kuua. Ila kuna baadhi ya watuhumiwa wanaowapeleka mahakamani lakini baada ya muda wanaachiwa aidha kwa dhamana au kesi kufutwa. Hapo ndipo panaleta shida. Panaleta shida kwa sababu baada ya muda mfupi unatokea tena ujambazi na waki-scan finger print wanakuta ni wale wale ambao ama wana dhamana au wameachiwa kwa kisingizio cha kuwa hawana hatia. Njia rahisi wanayoweza kufanya kukomesha lawana kutoka kwa wananchi ni control by elimination au killing. Njia hii ni nzuri sana kwa developing world kama zetu, ila tatizo akitokea mtu kama Zombe ndiyo inakuwa balaa!
Kwa kifupi huwa siwalaumu kabisa police kwa vintendo vyao
Mara nyingi sana Police huwa lengo lao siyo kuua. Ila kuna baadhi ya watuhumiwa wanaowapeleka mahakamani lakini baada ya muda wanaachiwa aidha kwa dhamana au kesi kufutwa. Hapo ndipo panaleta shida. Panaleta shida kwa sababu baada ya muda mfupi unatokea tena ujambazi na waki-scan finger print wanakuta ni wale wale ambao ama wana dhamana au wameachiwa kwa kisingizio cha kuwa hawana hatia. Njia rahisi wanayoweza kufanya kukomesha lawana kutoka kwa wananchi ni control by elimination au killing. Njia hii ni nzuri sana kwa developing world kama zetu, ila tatizo akitokea mtu kama Zombe ndiyo inakuwa balaa!
Kwa kifupi huwa siwalaumu kabisa police kwa vintendo vyao