Polisi yaua watuhumiwa wanne wa ujambazi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
WATU wanne wanaotuhumiwa kuwa majambazi wameuawa na Polisi mkoani hapa walipokuwa wakifanya jaribio la kutoroka mikononi mwa polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zelothe Stephen alisema jana kuwa watuhumiwa hao walijeruhiwa juzi saa tano usiku katika mtaa wa Chinyele Kata ya Nzuguni nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma na walikufa walipokuwa wakikimbizwa hospitalini.

Kamanda Zelothe alisema watuhumiwa hao wapatao sita wakiwa na silaha mbalimbali zikiwemo za kivita aina ya SMG na shotgun, walivamia duka la mfanyabiashara ambaye jina lake limehifadhiwa na kupora kiasi cha Sh laki tano na bidhaa mbalimbali zikiwemo simu tatu za mkononi.

Alifafanua kuwa uporaji huo ulifanyika mara baada ya majambazi kufyatua risasi kadhaa katika eneo hilo na kumjeruhi mfanyabiashara huyo kwa chupa ya bia kichwani.

Wakati polisi wakiwasili eneo la tukio, walikuta majambazi yalishatoweka katika eneo hilo ambapo waliokota maganda mawili ya risasi zilizotumika na risasi moja ambayo ilikuwa haijatumika.

Kamanda Zelothe alisema Polisi ilipata taarifa za siri zilizotolewa usiku huo na kuanzisha msako mkali uliofanikisha kuwapata watuhumiwa hao wakiwa wamejificha katika nyumba moja eneo la Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.

Alisema kati ya watuhumiwa hao, alikamatwa mtuhumiwa mmoja wa ujambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Shedrack William ambaye ni mkazi wa Mpama katika Manispaa ya Dodoma.

Kamanda Zelothe alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa muda mrefu kwa tuhuma za ujambazi uliofanyika mwaka jana eneo la Fufu wilayani Chamwino.

Nyumba ambayo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wamejificha ilipekuliwa ambapo bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba 56-396-6946 na magazini moja ndani yake ikiwa na risasi tatu ilikamatwa.

Pia polisi ilikamata baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuwa ziliporwa dukani kwa mfanyabiashara huyo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Zelothe, wakati polisi wakihojiana na watuhumiwa hao walikubali kuwapeleka polisi sehemu ambapo silaha nyingine ilikuwa imefichwa katika eneo la Nzuguni jirani na sehemu inayodaiwa kuwa uhalifu huo ulifanyika.

Alisema kwenye eneo hilo jirani na shamba la mahindi, watuhumiwa hao walionesha silaha aina ya shotgun iliyokuwa imekatwa mtutu na kitako na kufutwa namba zake.

Mbali na silaha hiyo, zilipatikana risasi 17 za bunduki hiyo na risasi 68 za SMG ambavyo vilikuwa vimefungwa kwenye mfuko wa sandarusi.

Wakati polisi wakipekua eneo hilo kwa makini, watuhumiwa hao wa ujambazi wanadaiwa walijifanya wanataka kukaa chini na kisha wakajaribu kukimbia katika shamba la mahindi kuelekea maeneo tofauti, hali iliyowafanya askari kufyatua risasi hewani.

Kamanda Zelothe alisema wakati askari wakiendelea kufyatua risasi hewani, watuhumiwa hao walizidi kutokomea ndipo walipolazimika kuwajeruhi ili kuwatia nguvuni na kuwakimbiza hospitalini ambapo daktari alithibitisha kuwa tayari walikwishakufa.

Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa utambuzi na taratibu nyingine za kisheria.

Polisi imetoa mwito kwa wananchi mkoani hapa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili kukomesha vitendo hivyo
 
This is no longer news. Same story, copy and paste kinachobadilishwa ni mkoa, rpc na idadi ya majambazi. Ukisoma between lines haileti sense hata kidogo

1. Majambazi wanne kwenda kuonesha silaha moja, was it necessary.

2. Kama tayari walikuwa na silaha kwa nini polisi walienda kichwa kichwa
porini kuoneshwa silaha, waliwaamini vipi hao. Polisi hawakuwa wanaweka
maisha yao at risk.

3. Kwa nini majambazi wasifungwe pingu, au polisi wanasubiri matokeo ya
tume ya pingu za Muro?

4. Walilazimika kuwajeruhu kwa namna gani na polisi walikuwa wangapi
kwenye operesheni hiyo.

Waandishi wa Dodoma mnaweza kufuatilia leads hizo, mtapata story kabambe i swear. Achaneni na press statement za polisi ni kutunga.
 
kwani polisi wanatakiwa kuwapiga risasi sehemu gani wahalifu wanaojaribu kutoroka?
 
Kwa kutumia common sense, inakuwaje unamkamata mtuhumiwa wa ujambazi unamuacha akitembea free, si hata wangefunga kamba? Lingine linaloshangaza, hivi hawa polisi wetu wanafundishwa kuua au kukamata. Kama kungekuwa na majibizano ningeelewa, maana hiyo ni vita. Watu wanne wanaokimbia, wote wanapata majeraha ya kusababisha vifo? Kuna jambo linalofichwa hapa.
 
Mzawa, hapo ndipo maumivu ya kichwa yanapoanza.
 
kwani polisi wanatakiwa kuwapiga risasi sehemu gani wahalifu wanaojaribu kutoroka?

Kazi ya polisi ni kuarrest offenders sio kuua offenders, hawatakiwi kupiga risasi, kirungu au fimbo. Nguvu ya ziada inatakiwa kutumika pale tu mtu anapo resist arrest. Kukimbia bila kutumia silaha kwa askari hakuwezi kujustify polisi kutumia silaha. Moja ya mafunzo ya polisi ni kukimbia na kwenye operesheni za namna hii mbwa ni muhimu sana, tunategemea kuwa polisi wangeanza kufukuza hao wezi na mbwa na kupuliza filimbi kama ilivyokuwa enzi za kina Hamza Azizi.

Kutumia silaha inamaanisha kuwa polisi hawawezi kukimbia, shauri ya vitambi, maybe.
 
ni muhimu zikawepo jitihada za ziada kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanakamatwa hai na kufikishwa mbele ya sheria badala ya kupoteza uhai. Hata hivyo, kinachotakiwa kuanzia sasa ni kukaza buti ili kuhakikisha kuwa usalama wa raia uko mikononi mwa polisi na uhalifu wa aina yoyote usipewe nafasi.
 
Askari wetu hawana mazoezi na mbinu za kukabiliana na wahalifu. wao wnachoweza ni kutumia silaha tu.
 
Hii inatisha kweli. Hao polisi wanatakiwa wafikishwe mahakamani lazima wana kesi za kujibu, uzembe, kutokua makini kazini na kusababisha vifo. Habari yenyewe ilivyokaa ni ya kutunga. hii ni Zombe stail.
 
Kiongozi,

Zombe style haikuanza leo. Ni model ya muda mrefu sana na very common ktk nchi nyingi zinazopenda shortcut na kutowajibika.
 
Staili ileile ya akina Zombe. Lakini whats is new here?

Kama ni hivyo tuendelee kukaa kimya ? Asasi za kirai za haki za binadamu zi wapu? Hata mtuhumiwa ana haki zake. Mpaka lini tutaendelea na dhana kuwa haki ya mtuhumiwa ni kuuwawa?
 
This is no longer news. Same story, copy and paste kinachobadilishwa ni mkoa, rpc na idadi ya majambazi. Ukisoma between lines haileti sense hata kidogo

1. Majambazi wanne kwenda kuonesha silaha moja, was it necessary.

2. Kama tayari walikuwa na silaha kwa nini polisi walienda kichwa kichwa
porini kuoneshwa silaha, waliwaamini vipi hao. Polisi hawakuwa wanaweka
maisha yao at risk.

3. Kwa nini majambazi wasifungwe pingu, au polisi wanasubiri matokeo ya
tume ya pingu za Muro?

4. Walilazimika kuwajeruhu kwa namna gani na polisi walikuwa wangapi
kwenye operesheni hiyo.

Waandishi wa Dodoma mnaweza kufuatilia leads hizo, mtapata story kabambe i swear. Achaneni na press statement za polisi ni kutunga.

Mara nyingi sana Police huwa lengo lao siyo kuua. Ila kuna baadhi ya watuhumiwa wanaowapeleka mahakamani lakini baada ya muda wanaachiwa aidha kwa dhamana au kesi kufutwa. Hapo ndipo panaleta shida. Panaleta shida kwa sababu baada ya muda mfupi unatokea tena ujambazi na waki-scan finger print wanakuta ni wale wale ambao ama wana dhamana au wameachiwa kwa kisingizio cha kuwa hawana hatia. Njia rahisi wanayoweza kufanya kukomesha lawana kutoka kwa wananchi ni control by elimination au killing. Njia hii ni nzuri sana kwa developing world kama zetu, ila tatizo akitokea mtu kama Zombe ndiyo inakuwa balaa!

Kwa kifupi huwa siwalaumu kabisa police kwa vintendo vyao
 
Polisi hawa bado wanafanya upelelezi wa kesi waliofungua ya ajali ya mbunge wa Kyela? IGP Mwema has his work cut for him!!
 
Mara nyingi sana Police huwa lengo lao siyo kuua. Ila kuna baadhi ya watuhumiwa wanaowapeleka mahakamani lakini baada ya muda wanaachiwa aidha kwa dhamana au kesi kufutwa. Hapo ndipo panaleta shida. Panaleta shida kwa sababu baada ya muda mfupi unatokea tena ujambazi na waki-scan finger print wanakuta ni wale wale ambao ama wana dhamana au wameachiwa kwa kisingizio cha kuwa hawana hatia. Njia rahisi wanayoweza kufanya kukomesha lawana kutoka kwa wananchi ni control by elimination au killing. Njia hii ni nzuri sana kwa developing world kama zetu, ila tatizo akitokea mtu kama Zombe ndiyo inakuwa balaa!

Kwa kifupi huwa siwalaumu kabisa police kwa vintendo vyao

Are you serious????????? Kwa nini wanaachiwa na mahakama?? Definately ushahidi unakuwa hautoshi na dhamana ni haki yao.

Kwa hiyo polisi wanakamata watuhumiwa, wanaenda IB wanalinganisha fingerprints wanaona zinafanana na za majambazi walioachiwa, wanawapeleka porini halafu wanawauwa.

With this kind of reasoning ujambazi hautakwisha.
 
Mara nyingi sana Police huwa lengo lao siyo kuua. Ila kuna baadhi ya watuhumiwa wanaowapeleka mahakamani lakini baada ya muda wanaachiwa aidha kwa dhamana au kesi kufutwa. Hapo ndipo panaleta shida. Panaleta shida kwa sababu baada ya muda mfupi unatokea tena ujambazi na waki-scan finger print wanakuta ni wale wale ambao ama wana dhamana au wameachiwa kwa kisingizio cha kuwa hawana hatia. Njia rahisi wanayoweza kufanya kukomesha lawana kutoka kwa wananchi ni control by elimination au killing. Njia hii ni nzuri sana kwa developing world kama zetu, ila tatizo akitokea mtu kama Zombe ndiyo inakuwa balaa!

Kwa kifupi huwa siwalaumu kabisa police kwa vintendo vyao

Mkuu, asante sana kwa kunikuna!
I wish ningekua askari polisi.

Niwe ninauhakika nimemkamata mhalifu ktk ujambazi na face to face napambana nae au ananikimbia, amepora mali za innocent person(s), ameua innocent person(s), kweli kweli wanajamii wallahi nisingemwachia m2 huyu.

Nani kawaambia mahakamani kuna haki. Haki? Giv me a break people. People innocent kabisa wanakufa na kuporwa na mali kijingajinga tu na wa2 ambao wanatafta shotikati ya maisha. Wtf

Kill em. I wuld too if i were a police.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom