Polisi yachunguza mlipuko ofisi za wanasheria (IMMMA Advocates)

Polisi yachunguza mlipuko ofisi za wanasheria (IMMMA Advocates)

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Dar es Salaam. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.

Mkondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.

“Tupo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama bomu limehusika,” amesema Mkondya.

Ameeleza hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.

“Tuwaachie Jeshi la Polisi wafanye kazi yao,” amesema Magai.

Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.

Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

- Mwananchi

News Alert: - DAR: Ofisi za IMMMA Advocates zawaka moto!
 
Kaka uchunguzi hapa Tanzania [emoji40]....! wengi wasio na makosa
 
Back
Top Bottom