Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Polisi nchini kenya imesema itatumia nguvu kupita kiasi kwa wale
watakao fanya maandamano ya kuitaka tume ya uchaguzi IEBC kujiuzulu.
Muungano wa upinzani CORD ukiendelea kusisitiza kuwa utafanya maandamano yake dhidi ya Makamishina wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC leo Nairobi na maeneo tofauti,kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Japheth koome ametoa onyo kali dhidi ya wale watakao shiriki maandamano hayo.
Kamanda huyo wa polisi aliyezungumza na vyombo vya habari jana alisema kuwa idara ya ujasusi imetoa ripoti kuwa Kuna mambo yamepaniwa kufanywa wakati wa maandamano yanatishia usalama wa jiji na taifa kwajumla.
Koome amesema kuwa kikosi chake cha usalama kiko tayari kwa vyovyote vile kukabiliana na waandamanaji wakaojitokeza kwani wanaathiri uchumi wa taifa kutokana na maandamano hayo.
Serikali kupitia idara ya polisi inasema kuwa muungano wa CORD unapasa kutilia maanani uamuzi wa uliotolewa na mahakama.
Hata hivyo mahakama kupitia kwa jaji Isaac lenaola ilisema kuwa waandamanaji wanapaswa kufanya maandamano bila kuathiri mtu yoyote, kuleta uharibifu katika ofisi ya IEBC au kuzua fujo jijini kwa njia yoyote ile uamuzi unaoonekana kuwakanganya wengi ikiwemo Serikali na upande wa upinzani,unashikilia kuwa mahakama imewaruhusu kuandamana huko Serikali ikisema uamuzi huo unapinga maandamano hayo.