Polisi washindwa kumhoji Gwajima

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,111
Reaction score
34,940
KWA UFUPI

  • Ni baada ya kuonekana hali yake bado haijaimarika

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana lilishindwa kuendelea kumhoji Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu tuhuma za kumtukana Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Askofu Gwajima alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jana asubuhi,ikiwa ni siku mbili tangu aliporuhusiwa kutoka katika Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Wakili wa askofu huyo, John Mallya alisema jana kuwa mteja wake alifika kituoni hapo saa 2.10 asubuhi, lakini Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam alipomuona, alisema hawawezi kumhojiano kwa kuwa afya yake haijaimarika.

“Alitutaka turudi na badala yake kufike kituoni hapo Aprili 9, mwaka huu,” alisema Wakili Mallya aliyeongozana na Askofu Gwajima pamoja na wachungaji wanane wa kanisa hilo.

Askofu Gwajima alijisalimisha mwenyewe kituoni hapo Ijumaa iliyopita, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Jeshi la Polisi, akituhumiwa kumkashfu Kardinali Pengo wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, wakati akiendesha ibada kanisani kwake.

Awali, wakati akihojiwa, aliishiwa nguvu na hatimaye kupoteza fahamu, hivyo kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema Askofu Gwajima lazima atahojiwa na ofisi yake ili kujiridhisha zaidi na shughuli anazozifanya, ikiwamo umiliki na uhalali wa kutumia eneo la Kiwanja cha Tanganyika Packers, kilichopo Kawe.

Makonda aliyezungumza kauli hiyo akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani hapo, alisema lengo la uamuzi huo ni kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.chanzo.Polisi washindwa kumhoji Gwajima - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Wewe makonda hujielewi.,eneo hilo hujui kapewa na boss wako hata kabla hujawa dc...leo unajifanya kiherehere,ulaaniwe kwa jina la yesu
 
Hii kesi kwa sababu inamhusisha KAFIR itamalizwa kimya kimya...kwa kuwa hata hao wanaomhoji ndio wale wale lakini kosa hili hili angelifanya muislamu kungezuka mengi sana na dunia nzima ingefahamu kupitia vyombo vyao vya habari..lengo likiwa ni kuupa uislamu taswira mbaya machoni mwa jamiii........
 
Makonda ni Mpum.bavu sana!. Sijui wamelipata wapi hili limbukeni la namna hii kuliweka kwenye ofisi ile? Kinondoni ondoeni hii bughudha isyokuwa na kazi za kufanya zaidi ya show.
 

Hizo ni fikra potofu na hazina mashiko,unaweza kuthibitisha ulichosema? acha kuendekeza dhana za udini! Ni bora ya mtu mwenye tongotongo za uso kuliko mtu mwenye tongotongo za fikra kama wewe!
 

Hivi hatuwezi kuwa na argumentation zinazo-base kwenye nadharia/theories au facts nyingine zaidi ya hii ya "ubinafsi" wa Ukristo na Uislam?

Thanks God ni Mkristo kwa Mkristo
 
Hizo ni fikra potofu na hazina mashiko,unaweza kuthibitisha ulichosema? acha kuendekeza dhana za udini! Ni bora ya mtu mwenye tongotongo za uso kuliko mtu mwenye tongotongo za fikra kama wewe!
Mbona unaandika kama vile unaumwa dege dege..........
 

Mmejengwa katika misingi ya chuki kwa wasio wa dini yenu, chuki imekukaba, unafaa ukaishi somalia kwa magaidi wenzio.
 
Mmejengwa katika misingi ya chuki kwa wasio wa dini yenu, chuki imekukaba, unafaa ukaishi somalia kwa magaidi wenzio.

Mbona hata nyinyi mnawachukia waislamu....na mnatamani hata wangefutika katika uso dunia hiii.....??
 
Wewe makonda hujielewi.,eneo hilo hujui kapewa na boss wako hata kabla hujawa dc...leo unajifanya kiherehere,ulaaniwe kwa jina la yesu

Ndugu usilitumie Jina la Bwana Yesu vibaya soma warumi 12:14
 
We ----- kweli! Hv ktk makundi yoyote ya Kigaidi dunia nitajie kundi la kikristo lolote! Ya ki islam bila hata kumiza kchwa kuna Alshabab+alqaida+boko haram na hata wale muslim brotherhood!. Na mnawashambulia wakrsto sasa nani mwenye chuki?
 

mkuu mbona unaleta mambo ya udini hapa?
 
Makonda ni Mpum.bavu sana!. Sijui wamelipata wapi hili limbukeni la namna hii kuliweka kwenye ofisi ile? Kinondoni ondoeni hii bughudha isyokuwa na kazi za kufanya zaidi ya show.

jamani muacheni makonda afanye kazi yake sawa .mbona mna hasira sana?
 
Niukweli usio pingika Gwajima angekikua Sheik wa kiislam asingetokaa
 
Makonda hamna kitu kabisa ndani ya fuvu lake...

Kuwa Mwenyekiti w Ulinzi na Usalama sio kigezo cha kufanya kazi za ukachero...

Naona anachanganya mambo huyu zumbukuku, yeye ni administrator na kama ana wasiwasi na dukuduku atoe amri kwa makachero wafanye hayo anayotaka kufanya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…