Polisi wanatumia vigezo gani kukamata walevi na wazururaji mjini Katesh?

rr4

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
3,338
4,649
Ni sawa mnavotaka kila mtu awajibike lakini angalieni njia mnayotumia.

Leo nimeona kitu unique sana hapa Katesh na kinaendelea muda huu. Nawapongeza kwa kukamata wazururaji na walevi ila nguvu inayotumika ni kubwa mno. Watu wanapigwa sana na kudhalilishwa kama wanyama.

Kuna wengine wapo nje ya ofisi mbalimbali wamepigwa na kurukishwa kichura, wanakopelekwa hapajulikani maana sidhani kama rumande ya Katesh inaweza kuhimili wote.

Please jengeni uwajibikaji ila sio kwa staili hii ya jeshi lako la polisi. Wako kama wamevuta ndo wakaingia mzigoni.

Kinachofanyika ni udhalilishaji.
 
HAPA KAZI TUU..hakuna kuzurula mchana wala kunywa pombe hasa isiyo na TBS wakati wa kazi. Kaa hao walishafanyakazi ndio wakaenda kunywa shauri yao haijalishi ila muda ni jioni ule aliopanga mheshimiwa tuu..
 
Katafute kazi ufanye acha uvivu, sisi ndiyo tunataka hivyo, kujenga nchi siyo lele mama, unafikiri nchi inajengwa kwa kuzungusha mkono?

Kama hautaki, hama nchi!
 
Umeisoma vizuri post??????? Nimepongeza jitihada zinazofanyika ila nimesema njia inayotumika ni ya kidhalilishaji. Mimi niko kwenye ofisi flani hapa, kuna watu nje wametoka kijijini Gehandu nasikia ni karibu na Singida huko mara wamekunjwa na kichura juu na wamechanganywa na walevi na sasa tunasikia kwa ajili ya udogo wa rumande wengine wanapelekwa BABATI.

Je ni sawa????????????? Sio kumpotezea mtu muda huko. Na pesa Kwasababu atahitaji nauli ya kurudi kwao.

Polisi wasiwe maroboti. Mlevi anajulikana na mtu mwenye shughuli zake anajulikana.
 
Katafute kazi ufanye acha uvivu, sisi ndiyo tunataka hivyo, kujenga nchi siyo lele mama, unafikiri nchi inajengwa kwa kuzungusha mkono?

Kama hautaki, hama nchi!

Tumia akili. Hapa ni kazini bwana mdogo na naifanya haswa. Ukamataji ni wa kidhalilishaji sana waliofanyiwa hawa raia wasio na hatia. Piga picha unaelekea Benki kutoa hela then unadakwa na kupigwa kama mbwa.
 
Hawo ni wazurulaji, Askari wetu huwa hawamuonei mtu, kama wewe ni raia mwema na unatii sheria za nchi yetu bila ya shurti hakuna wa kukubughudhi!
 
Ina maana wanakamata kila wanayekutana nae!!?

Ndo ivo Mkuu. Just imagine hauulizwi kitambulisho au unafanya kazi gani. Wengine wapo hapa kununua mazao na kadhalika na mtu akikutetea kwamfano.... akasema huyo sio mdhururaji ni hivi na hivi................ na yeye anachanganywa.

Kinachofanyika ni sawa ila njia ni very primitive.
 
Kazi bado ipo kuwaandaa watanzania wote kufanya kazi.

Wala kazi si kubwa, watenge mapori yawe na:
1. Usalama

2. Maji

3. Malazi

4. Barabara

5. Maeneo ya kutosha ya kulima au kufuga

6. Masoko yawekwe wazi na vya ndani vithaminiwe kuliko vya nje, Mzawa auze kwanza.

Then wakamatwe wasio na kazi, wapiga debe na walevi wapelekwe huko.

Kama mtu wamezaliwa wanaume 7 na baba ana heka moja na hawakusoma wote unategemea nini.????

Hili suala ni zuri ila linatakiwa lisikae kisiasa tu. Kiongozi anaamka nasema leo wakamatwe wazembe na wazururaji then what.

Maana ukiwapeleka jela au rumande bado watakachokula ni kodi yetu na hivyo hatusongi.

Miundombinu ya makambi iandaliwe then wakamatwe.
 
Wakazi wa Manyara huwa muda mwingi (hasa wanaume) hawakosi kushika fimbo mkononi, sasa hizo fimbo niza nini mie nilijua ni kwa ajili ya kujihami!
 
We.... Mziki wa vijana wa CCP sio mdogo, nadhani ndo wametoka depo. Halafu ni wengi mno na Makarandinga meupe.
 
HAPA KAZI TUU..hakuna kuzurula mchana wala kunywa pombe hasa isiyo na TBS wakati wa kazi. Kaa hao walishafanyakazi ndio wakaenda kunywa shauri yao haijalishi ila muda ni jioni ule aliopanga mheshimiwa tuu..
Kwa hiyo mimi mlinzi naingia job saa 10 ninywe pombe saa ngapi...?
 
Ndo ivo Mkuu. Just imagine hauulizwi kitambulisho au unafanya kazi gani. Wengine wapo hapa kununua mazao na kadhalika na mtu akikutetea kwamfano.... akasema huyo sio mdhururaji ni hivi na hivi................ na yeye anachanganywa.

Kinachofanyika ni sawa ila njia ni very primitive.

Hiyo ndiyo shida mmojawapo ya wanausalama wetu! Elimu ya kusimamia maagizo ni shida kidogo! Bado wako na munkari ule wa kutokea CCP Moshi. Mtindo huu wa kugeuza kila anayekuwa barabarani au sehemu ya kilevi kuwa mlevi haiko sawa hata kidogo. Ebu chukulia mfano. Unashida na mlevi na umeamua kumfuata huko kilabuni wakati uko kwenye hiyo eneo unakumbana na kamatakama hii- Nadhani wanausalama wanatakiwa kuendesha shughuli hii kiustaarabu na kwakuwashirikisha viongozi wa serikali za Mitaa.
 
Back
Top Bottom