Polisi waliowauwa watu weusi Marekani kutoshtakiwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Idara ya sheria Marekani inaarifiwa kuamua kutowashtaki maafisa wawili wa polisi waliompiga risasi na kumuua mwanamume mweusi huko Louisiana mwaka jana.

Kanda ya video inaonekana kuwaonyesha maafisa hao wazungu wakimzuia chini Alton Sterling walipofyatua risasi, hatua iliozua maandamano ya siku kadhaa huko Baton Rouge.

Misa ya kumbukumbu inafanyika katika eneo alipouawa.

Afisa mwingine wa polisi mzungu nchini Marekani aliyepigwa picha akimpiga risasi mgongoni mwanamume mweusi ambaye hakujihami miaka miwili iliyopita amekiri makosa ya ukiukaji wa haki za raia.

Huenda afisa Michael Slager akahukumiwa maisha gerezani kwa kumuua Walter Scott.

Chanzo: BBC Swahili
 
Kama unataka kuche zile video mtafute the game istagram .....wazungu wana hate sana
 
Siye kazi yetu kuwashobokea pale wajapo afrika ,wazungu , waarabu, wadosi, waisrael na watu weupe wote ni wabaguzi
Nalog off
 
wale wapenzi nyuzi kama hizi hawagusi ila nikusifia tu aaah us ana siraha nzuri za kivita kuliko North Korea
 
wale wapenzi nyuzi kama hizi hawagusi ila nikusifia tu aaah us ana siraha nzuri za kivita kuliko North Korea
Hapo sasa ndio shida ya sisi wabongo na wafrica kwa ujumla kila kitu ni kufurahia cha wamarekani na mifano ni mingi humu JF. Lakini mtoa mada angeibalisha kichwa cha habari na kuweka kama hv " polisi wa kiarabu walioua watu weusi arabuni kutoshitakiwa" daah asee angepata view na wachangiaji wengi sanaaaa.

Iko mada moja murua kabisa ilitumwa humu jf ikielezea ya kwamba wafrica akili yao ni fresh kabisa haijatumiwa kabisaaaa. Mfano unayo gb 1000 ya hard disk na unaitumia kwa ujazo wa gb 1. Na huo ujazo ni vitu tulivyokaririshwa ama makanisani au misikitini.

@terible teens
 
Back
Top Bottom