Kamanda wa polisi wa wakati ule kutoka mkoani Dodoma alikana kuwa hamna askari kutoka mkoani kwake aliyepelekwa Iringa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma wa sasa Ndugu David Misime anasema hana taarifa kuhusu malipo hayo hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni mgeni mkoani humo na hajui chochote kuhusu askari walioenda huko Iringa, sasa hapa ni nani wa kumwamini kati ya polisi waliotoa malalamiko au ni makamanda wao?
Ila ripoti ya kamati Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyoundwa na kuchunguza tukio hilo ambalo lilipelekea kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi , ilisema Mwangosi aliuawa kwa makusudi na polisi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.
Je,kamati iliyoundwa na Jeshi la polisi inasemaje?