Polisi Morogoro wakithiri kwa rushwa

Balile

Member
Oct 10, 2011
74
140
Ndugu zangu uonevu umezidi katika nchi hii. Polisi Morogoro wanatisha. Kijana Fredy Mgaya anateseka rumande kwa kukosa rushwa.

Novemba Mwaka Jana Mke wa Rafiki yake, alikwenda nyumbani kwake. Akamwambia wamegombana na mumewe akasaidie kusuluhisha. Alipofika akakuta watu kadhaa, mara wakamkamata. Wakasema ameiba Pikipiki.

Alikamatwa Nov, 2014. Yuko ndani Polisi Ifakara. Polisi aitwaye Dulla anadaiwa kupokea 500,000 kutoka kwa Mzee Mapunda, akawaachia Vijana watatu waliokamatwa pamoja na Fredy.

Fredy wamemtaka mama yake awape hela akawa hana. Wamembambikia kesi January, Hakimu akaifukuza, sasa ingawa alikuwa ndani tangu Novemba. Sasa wanasema ameiba jenereta January 2015 (akiwa ndani).

Polisi wamemwambia dhamana yake imefungwa mahakamani na waliokwenda kumdhamini- Swaga na Kipanga Pori, polisi wamewakamata na wanataka kila mmoja atoe 30,000 waachiwe.

Askari anayeitwa bonge, Jumanne Aprili 14, ndiye aliwaweka ndani Kisha akawatoa baada ya kumpa rushwa Sh 32,000.

Kamanda wa Polisi Morogoro anayo taarifa hii, lakini ameweka pamba masikioni. Waungwana msaidieni huyu mnyonge.

Balile
 
Back
Top Bottom