Polisi kuchunguza kisayansi tukio la anayedaiwa kufariki na kuonekana akiwa hai tena Geita

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na mamlaka zingine ikiwemo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali limeanzisha uchunguzi wa kisayansi kuhusu uvumi na madai ya kijana Nyabongo Manosa (19)anayedaiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wa Malaria June 7 mwaka 2013 na kuzikwa June 8 katika kijiji cha Mpunze wilayani Meatu lakini akaonekana Septemba 14 mwaka 2015 katika kitongoji cha Iroganzala kata ya Masumwe wilayani Mbogwe mkoani Geita akiwa hai.

Baada ya tukio hilo kujitokeza Manosa Benjamini mwenye umri wa miaka 44 aliyejitambulisha kuwa mkazi wa kijiji cha shinyanga A kata ya Nyakafuru wilayani Mbogwe na mkewe walijitokeza na kudai ni mtoto wao aliyefariki mwaka 2013 kwa malaria ambapo walikabidhiwa kijana huyo kupitia Ofisi ya Ustawi wa jamii wilaya ya Mbogwe wakati uchunguzi wa kina ukiendelea.

Matokeo ya uchunguzi huo yatakamilika ndani ya wiki mbili zijazo ambayo yatahitimisha uvumi na madai hayo kwa kubainisha ukweli iwapo kijana huyo alifariki na kisha kufufuka tena au la.
 
Back
Top Bottom