Tarehe 5 Januari 2011, zilitokea vurugu katika jiji la Arusha zilizosababishwa na jeshi la polisi kuzuia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na wananchi wengine kutembea kwa miguu kwenda katika mkutano wa hadhara uliopamgwa kufanyika katika viwanja vya Unga Limited.
Jeshi la polisi lilikuwa na habari na mkutano huo na waliahidi kuwepo ili kulinda usalama.
Siku chache kabla ya mkutano huo kufanyika viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha walitoa taarifa ya nia ya kufanya maandamano pia.
Polisi waliwaandikia barua ya kukubaliana na nia hiyo na kuwahidi kutoa ulinzi katika maandamano hayo.
Lakini siku moja baada ya maandano hayo kuruhusiwa, mkuu wa jeshi la polisi alionekana kwenye vyombo vya habari akisema, “Maandamano hayo yamezuiwa.”
Kauli hiyo haikueleweka kwa viongozi wa CHADEMA kwa sababu hakuwa na mawasiliano ya maandishi yaliyofikishwa katika chama CHADEMA yakibatilisha ile barua yao ya awali iliyokubali maandamano.
Hivyo, uongozi wa CHADEMA taifaifa, kutokana na kibali hicho cha awali, ulishasafiri kwa ndege na usafiri mwingine kwenda Arusha kushiriki katika tukio hilo.
Kufuatia kauli ya mkuu wa jeshi la Polisi (IGP), uongozi wa CHADEMA uliamua kusitisha maandamano hayo, huku wao wenyewe wakiamua kutembea kwa miguu kwenda kwenye viwanja vya mkutano.
Baadhi ya wananchi na wanachama waliamua kutembea pamoja na viongozi wao. Walitembea hivyo kwa takribani kilomita mbili, wakisindikizwa na polisi wa doria na wa kawaida.
Matembezi hayo yaliendelea kwa umbali huo kwa utulivu na amani kubwa mpaka walipofika sehemu inayoitwa Sanawari ambapo polisi waliamua kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto zilizojeruhi wananchi kadhaa na kuuwa wengine bila hatia.
Kimsingi yaliyotokea hapo ni mengi na mengine yameandikwa katika vyombo vya habari.
Yalikuwa maandamo ya kupinga utaratibu mbovu uliotumika kumuweka Meya wa kichina kwa wakati huo
Leo hii Mungu amesikia kilio chetu na kuwafutilia mbali wakandamizaji wa demokrasia Arusha yani namaanisha CCM,.
Leo tunaongoza jiji la Arusha Meya na Naibu Meya wanatoka Chadema,
Tulichokipigania miaka mitano nyuma Mungu amekijibu.
Hatukukata tamaa na Hatutakata Tamaa.2020 sio mbali kwa wamchao Mungu.
Pumzikeni kwa Amani watangulizi wetu.

Last edited by a moderator: