Polisi Dar yakamata ombaomba 45, 17 wapelekwa gerezani

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.jpg


Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamewakamata na kuwaondoa ombaomba 45 na 17 wamewapeleka gerezani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii, wanafanya utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani walikotoka.

“Kazi hii inaenda vizuri na ombaomba wachache wamebakia ambao wakiwaona askari wanakimbia na kutokomea kusikojulikana,”alisema Sirro.

Katika tukio lingine, Polisi wanawashikilia watuhumiwa 96 wenye umri wa miaka 15-18 wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya kuvamia nyumba na kuiba usiku.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao wanajulikana kwa jina maarufu la ‘kumi ndani kumi nje’, walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya jiji na wanaendelea kuhojiwa na polisi, upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.

“Watuhumiwa hawa wanavunja milango kwa mawe makubwa na kuiba televisheni na simu, upelelezi unaendelea na wanaendelea kutajana hivyo tutawakamata na wengine,” alidai kamanda huyo.

Wakati huohuo, Kamanda Sirro alisema makosa ya kuvunja Sheria ya Usalama Barabarani mkoani hapa, yameliingizia jeshi hilo mapato ya Sh463 milioni kwa muda wa siku 10.

“Jeshi la Polisi kazi yetu ni kusimamia sheria siyo kukusanya mapato, hivyo watu wazingatie sheria,” alisema kamanda huyo.

Alisema ili kupunguza matukio ya uhalifu, jamii haina budi kuhakikisha kunakuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao na Serikali za Mitaa zinapaswa kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa na linafanyika.
 
na huko mikoani watapokelewa ?
wengine walikua ombaomba kwa kukataliwa na ndugu hasa walemavu..
kama ni kero wangewatwanga tu risasi kama Mkapa alivyowafanya Wapemba.
 
Kumi ndani kumi nje..hichi kikundi hakina tofauti na askari wa usala barabarani wanao lazimisha kupiga fine watu..
 
Sheria gani wanayosimamia inayowafanya wawakamate ombaomba. Kwani kuomba ni kosa la jinai?
 
Huko grezani watalala ndani na kula bure kitu ambacho wanakililia kila siku.

Tuna kawaida ya kutumia nguvu nyingi ambazo mwishoni hazina tija. Kumuweka mtu mahabasu ni gharama. Sidhani kama wamefanya hesabu na kujua ni kiasi gani serikali inawagharimia hawa watu wasio wakosaji.
 
Sheria gani wanayosimamia inayowafanya wawakamate ombaomba. Kwani kuomba ni kosa la jinai?
......uzururaji.......

Nchi hii huweza kukosa kosa, sheria zipo kibao, ugaidi, utakatishaji fedha, makosa ya mtandao n.k
 
Idara ya ustawi wa jamii ni sehemu ya tatizo. Wana sera kazi kuhusu watu wasio na ajira? Ibara ya 14 ya katiba inatamka bayana " kila mtu anayo haki ua kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria", swali no kwa nini hawa watu hawapati hifadhi ya maisha yao, mpaka wanakua ombaomba ?
 
na huko mikoani watapokelewa ?
wengine walikua ombaomba kwa kukataliwa na ndugu hasa walemavu..
kama ni kero wangewatwanga tu risasi kama Mkapa alivyowafanya Wapemba.

Ndugu yangu Sharif unao uhakika na ushahidi unaojitosheleza mbele ya sheria kuwa katika uongozi wa huyo uliemtaja aliagiza au kutekeleza hivyo kwa Wapemba?Naomba tuutumie uhuru wetu kujiendeleza na kujifunza na tuachane na ushabiki haswa wa kisiasa na kuchafuliana majina.Huo ni ushauri tu kwako na wengine ikiwa unaona utakufaa.
 
Kifungu gani cha sheria kinakataza uzururaji. Halafu ukiulizwa uzururaji ni nini au elezea uzuraraji utajibu nini.
 
Wakati huohuo, Kamanda Sirro alisema ''makosa ya kuvunja Sheria ya Usalama Barabarani mkoani hapa, yameliingizia jeshi hilo mapato ya Sh463 milioni kwa muda wa siku 10."'

Nimeipenda hii tu ...!
 
Ndugu yangu Sharif unao uhakika na ushahidi unaojitosheleza mbele ya sheria kuwa katika uongozi wa huyo uliemtaja aliagiza au kutekeleza hivyo kwa Wapemba?Naomba tuutumie uhuru wetu kujiendeleza na kujifunza na tuachane na ushabiki haswa wa kisiasa na kuchafuliana majina.Huo ni ushauri tu kwako na wengine ikiwa unaona utakufaa.
usinifundishe uoga mkuu..
Mkapa ndie aliuwa Wapemba january 27 2001 wasiopungua 70..
narudia tena mauwaji ya Wapemba ya January 27 2001 yalifanywa na mkapa..
 
Kuna binaadamu asiyeomba mbona wao hao viongozi walikuja mjini kuomba kazi, wangekaa huko mikoani wakasubiri kazi ziwafuate majumbani mwao. Duniani kote ombaomba hawakosekani, hizo mbwembwe tu wakizoea madaraka watawaacha tu.
 
na huko mikoani watapokelewa ?
wengine walikua ombaomba kwa kukataliwa na ndugu hasa walemavu..
kama ni kero wangewatwanga tu risasi kama Mkapa alivyowafanya Wapemba.
Sharifu kumbuka kuna sheria ya makosa ya mtandao shauli yako.
 
nlikua namheshimu sana siro toka alivokua Mwanza,lkn sahii atatekeleza hadi amri ya diwani bila kufkria.baba angu siro toka huko uliko heshima yote wanasiasa wanakuondolea,huoni? wanaokupa hayo maagizo ya kunyanyasa maskini ndo wanashindwa kuwajibika baba angu! kesho sina hakika watakuagiza nn maskini!! umebaki kujibu maswali magumu wao wamekaa pembeni.
 
Back
Top Bottom