Ningefurahi kuona maelezo yanayotoa "facts" lakini bahati mbaya maelezo mengi yanatoa "feelings" inakuwa ni vigumu kuhukumu mtu kwa "hisia" na story imeandikwa upande mmoja tu je umeshaonana na wahusika ukawauliza kwa mfano polisi kwamba kwanini wanaendelea kushikilia hati hiyo? mbali na barua ya mahakama pengine kuna maelekezo toka ngazi za juu.Polisi hufanya kazi kwa utaratibu na si vinginevyo.Hutendi haki pale ambapo hujauliza upande wa pili kuthibitisha kilichosemwa ni kweli au la.Nadhani usiegemee kwa maelezo ya Mollel pekee nenda kwa wahusika waulize na kama hukuweza kuwahoji usitumie maneno ya Mollel kujaza nafasi ya mazungumzo yao na ndio maana nasema yaliyoandikwa ni hisia nyingi dhidi ya watu wengine, hisia hizo mwisho wa siku hazitajenga mahusiano mema.Mfano umemwandika king'ori vibaya mahusiano yake na mapenzi au mke hapa yanahushu nini ?
-Barua ya mwanashaeria inaonyesha apewe hati lakini bado imeonyesha kuna haja ya kufunguliwa kesi ya madai maana yake kuna tatizo hapo.na hii haimainishi asipewe hati.Lakini kuna uwalakini hapo.sasa vilevile muulize wakili wa serikali kwanini Makanga anshauriwa afungue kesi ya madai ? wao wanasheria wameona nini mpaka kutoa ushauri huo?Hali kadhalika nenda kwa polisi waulize kwa nini wanaendelea kushikilia hati hiyo? wakati ambapo kesi imekwisha? (Maelezo toka pande mbili hizi yatasaidia kupata upanana uelewa wa mabo jinsi yalivyo).
-Vilevile muhtasari unaodaiwa kughushiwa uwekwe hapa hadharani kama ilivyoweka barua ya mwanasheria ili tuweze kuona na kutoa maoni.Vilevile kama kuna orodha ya watu kwenye muhtasari basi nao wahojiwe wathibitishe wanautambua muhtasari na majina na sahihi ni za kwao na si vinginevyo.Ukifanya hayo haki itandeka na sisi wasomaji tutapata picha kamili.