GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Tangia huu ujio wa hizi Simu na hii Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania ni kama vile waliotuletea wametupulizia filimbi ya utovu wa nidhamu na kuwa Watu tusio na maadili.
Leo hii si jambo geni kwetu kuona Watu wakipiga tu picha hovyo hovyo huku zingine hata zikiwa hazina na kichwa wala miguu yaani sasa imekuwa ni kama vile kila Mtanzania ni mpiga picha yaani ni vurugu vurugu tu.
Kiini kikubwa cha uzi huu ni kutaka kuelezea tena kwa masikitiko makubwa tabia ambayo inazidi kuota mizizi ambapo pale panapotokea tu ajali ya gari na Watu labda wamepoteza maisha au kuna majeruhi baadhi ya Watanzania ambao nawaita Wapuuzi badala ya kutoa msaada wakati wa tukio husika kwa Walengwa wao muda wote huishia tu kupiga picha ama Maiti au wale Majeruhi kisha kuwahi kutuma katika Simu zao na Mitandaoni.
Baada ya kukerwa na hii nikaona isiishie tu hapo bali inabidi niwe natoa " dozi " kwa wenye hizi tabia ambapo majuzi tu Weekend ilinibidi nimpe mtu " nakoz " za maana baada ya kutokea ajali moja ya gari maeneo ya Boko na sisi tukakimbia kwenda kutoa msaada na pakawa na Sharobalo mmoja hivi ambaye yeye badala ya kuja kuungana na sisi kutoa msaada akawa anapiga tu picha na sikumvumilia na badala yake nami nikamtolea uvivu ambapo nilimpa kidogo " kichapo " cha haja na hatimaye akaenda kunishtaki Police.
Baada ya kupelekwa Police kwa kosa la kumpa " kipondo " yule Kijana kwa ule upuuzi wake nilijitahidi kujieleza kwa uzuri wake na mapana yake ambapo nilieleweka na kuachiwa huru kitu ambacho nilitafsiri kama ushindi mkubwa kwangu.
Nilichoamua sasa ni kutaka kuanzisha Kampeni maalum ambapo nitakuwa navizia tu ajali zinapotokea na nawahi eneo la tukio na endapo nitamuona tu Mtu badala ya kutoa msaada yeye ana " photoka " tu basi sitakuwa na namna zaidi tu ya kumpa " discipline " a.k.a kichapo hadi Watanzania tunyooke na tuachene na hii tabia mbaya na isiyokuwa na maadili.
Mwisho nitoe tu RAI yangu kwa Police Tanzania kuwa kama wakiwa wanapokea kesi za aina hii za Mtu kupigwa baada ya kuonekana anapiga picha Maiti au Majeruhi wakati wa ajali au mkasa basi wawe wanawaachia ( wanatuachia ) Watu waliopiga ( tuliopiga ) tena bila hata ya dhamana kwani kwa namna fulani hata sisi pia tunawasaidia wao ( Police ) kuwa na jamii yenye maadili, utu na heshima ambayo wao pia wanapambana nayo kila kukicha.
Na pia ningewaombeni na Watu wengine pia mkiwa mnaona tabia hii ipo huko ulipo usisite kutoa Dozi kwa " mphotokaji " ili tu tejenge nidhamu na adabu ili Watanzania baadhi waachane na hii tabia inayokera kwakweli.