Police dhibitini Mabasi ya shule Shinyanga

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,010
Mabasi haya yanaendeshwa spidi kubwa sana tena kati kati ya mji kiasi kwamba leo jioni basi moja la Hope kidogo ligonge mwendesha bodaboda akiwa na abiria.

Nimesikia baadhi ya watu wakiwa na hasira na tabia hii na wakasema siku moja watachoma moto basi litakalosababisha ajali kwani madereva hawa wa mabasi ya shule huwa kama wamevuta bangi na hawako makini barabarani

Nawaomba polisi wa usalama barabarani wawaite hawa madereva na kuwaonya tabia yao hiyo ya kutokuzingatia usalama wa watumiaji wengine wa barabara.Na ikibidi wakaguliwe iwapo kweli wana sifa ya kubeba watoto wetu kwenye mabasi hayo.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Madereva wetu tz hawaongozwi na alama za barabarani ila penye watu wengi ndo wanatafuta umaarufu aonekane
 
Back
Top Bottom