AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Viongozi na Watendaji wa Imani Media wameipongeza serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi ya kuwa hudumia watanzania na kuomba Serikali iendelee kushirikiana nao. Pia wametumia fursa hiyo kuelezea utendaji wao wa kazi kama Taasisi pamoja na shughuli mbalimbali wanazozifanya za kusaidia Jamii.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Amewasibitishia kuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi itaendelea kushirikiana nao katika kila Jambo Jema wanalolifanya na ipo kwaajili ya Watanzania wote.
Ndugu Humphrey Polepole amewapongeza Imani Media kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhabarisha umma juu ya habari mbalimbali pamoja na shughuli zao za kusaidia Jamii ikiwemo kuchimba visima, kusaidia wahanga wa majanga na Wagonjwa wenye uhitaji wa matibabu .
"Shukrani kwenu kwa kazi kubwa mnayoifanya, Msitosheke, Katika kutenda mambo mema hakuna kutosheka, Endeleeni kutenda mambo hayo".Amesema Ndgu Humphrey Polepole.
Chama Cha Mapinduzi kimeahidi kwa sasa kuendelea kushirikiana na Makundi ya kijamii mbalimbali ili kutafsiri dhana ya Chama Cha watu kwa vitendo.