MangwelaJr
Senior Member
- Jan 4, 2017
- 102
- 241
Chama cha Mapinduzi kimewashukuru watanzania kwa kukipa ushindi mkubwa katika chaguzi ndogo za madiwani na ubunge zilizofanyika mwishoni mwa wiki huku kikiweka hadharani siri ya ushindi.
Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za makao makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humprey Polepole amesema ushindi huo ni ishara tosha ya jinsi ambavyo watanzania wana imani na chama hicho, na kwamba kuna siri mbili kubwa zilizokipa chama hicho ushindi.
Siri ya kwanza aliyoitaja Polepole ni MAGEUZI ambapo uamuzi wa CCM kuzaliwa upya na kufanya mageuzi makubwa yanayolenga kukirudisha chama hicho kwa wanachama pamoja na kushughulika na shida na kero za watu umefanya watanzania wakielewe zaidi chama hicho.
Siri ya pili ya ushindi wa chama hicho kwa mujibu wa Polepole ni kazi nzuri ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ambaye tangu apewe dhamana ya kuiongoza Tanzania ametekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi nyingi nyingi alizoahidi ikiwemo ya kupambana na rushwa na ufisadi ikiwa ndiyo kazi ya kwanza aliyoanza nayo.
Polepole ametaja ahadi nyingine ambazo zimekuwa ni kivutio kikubwa na kuwafanya watanzania wakipe ushindi chama hicho ni utoaji wa elimu bure, ujenzi wa viwanda, miundombinu ikiwemo ununuzi wa ndege na zaidi ya yote kuwasikiliza wananchi na kero zao.
My take:
Humphrey Polepole anaendelea kupotosha umma kwamba ccm ni chama kinachopata mafanikio kwa kuwa kinaaminika na wananchi kwa uchapaji kazi wake na Sera zake kwamba zinatekelezeka kila kukicha..
Ukweli ni kwamba chama cha mapinduzi kinaendelea kudidimiza demokrasia nchini kwa kutumia mbinu ovu za rushwa,mabavu na hila dhidi ya vyama vya upinzani katika chaguzi mbalimbali.
Pia ccm na dola vimefanikiwa kuvitumia baadhi ya vyama vya upinzani na baadhi ya viongozi wake kama mamluki kugawa kura za upinzani kama njia ya mafanikio yao..
Wananchi tunaona yanayoendelea ndani ya ccm na dola katika kuminya demokrasia na haki ya wananchi katika kuamua nani awe kiongozi wao.