Kilichonifurahisha ni huo mswada wa sheria ambao naona ni ngumi ya usoni kwa Kibaki na Karua ambaye alipambana kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba ODM hawapati nafasi ya Executive PM. Sasa kama atabaki kwenye cabinet ajue wazi kwamba atatakiwa ku-report kwa Raila.
Mswada ni kitanzi kwa Kibaki kwa kuwa anajua wazi kwamba akim-frustrate Raila, ajue wazi kwamba ODM watajitoa kwenye coalition na hivyo ngoma itawekwa kati.vuruga makubaliano halafu ODM waka-walk out of coalition ajue wazi kwamba ngoma ikiwekwa kati hawezi kupata kitu tena. Maana ECK hawatarudia ujinga waliofanya mwaka jana kwa kuwa kasheshe yake wanaifahamu. Yaani Kibaki hana ujanja kabisa, inabidi atulie kama ananyolewa kwa wembe ama chupa maana akijitikisa kidogo tu ajue kwamba wembe utamkata!
Je, Kibaki kuonekana kanisani bila ya wapambe wake siku ya jumapili iliyopita ni dalili kwamba washikaji wake wa karibu wameanza kumtosa? Kama wamemtosa, je, hatima ya PNU ni nini? Is this the end of GEMA regime/era?
PNU wana hali ngumu sana na especially wale ambao walikuwa ni hardliners kama Michuki, Kimunya na Karua. Sijui watawezaje kufanya kazi na Raila ambaye walikuwa wanamsema vibaya plus some other Pentagon members ambao watakuwa kwenye cabinet.
Nina hamu sana ya kusikia msimamo mkali wa mtu kama Danson Mungatana ambaye nadhani alikuwa anahisi kwenye kujaza mapengo angekumbukwa na kupewa nafasi. Lakini ndoto hiyo sasa haipo tena.
Mtihani mgumu ni kwa Kibaki, je, atawabeba KANU na ODM-K? Ili kuwabeba kwenye coalition yake lazima awape nafasi za uwaziri ama naibu waziri. Ili hivyo vyama vingine (KANU na ODM-K) vipate mawaziri lazima baadhi ya washikaji kutoka GEMA watemwe, je ataweza kuwatema???????