Playoff: Coastal Union 3-1 Pamba (5-3) | Coastal Union yafanikiwa kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Timu ya ligi kuu, Coastal Union leo inacheza mechi ya marejeo na timu kutoka daraja la kwanza inayojaribu tena kurudi ligi kuu, Pamba ya Mwanza. Mechi iliyopita walitoka sare ya magoli 2-2 na mshindi yeyote wa mechi ya leo anaweka mguu ligi kuu.


========
00' Mpira unaanza hapa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga

10' ⚽ Pamba inaandika bao la kwanza baada ya mpira maridadi wa Fadhili Juma kuguswa na beki wa Coastal na kumpoteza mlinda mlango.

29' Mwamuzi ameipa penati Coastal faida ya mkwaju wa penati baada ya Majaliwa wa Pamba kumuweka chini mchezaji wa Coastal Union

31: ⚽ AbdulRahman Sopu anaiwekea Coastal bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penati

49' Edward wa Pamba anapewa kadi ya njano

42' Refa anafunika tuta la pili, mpira uligonga giganja cha mchezaji wa Pamba

43' Mlinda mlango Samuel Simon anapangua mkwaju wa Sopu na Coastal inashindwa kutumia faida.

68' Mabadiliko Coastal Union, Hamadi majimengi anachukua nafasi ya Issa

71' Coastal wanapata freekick kwenye mstari wa 18 wa Pamba

72' ⚽ Abdul Sopu anaweka bao la pili kwa upande wa Coastal

89' ⚽ Mlinda Mlango wa Pamba anajifungua baada ya kujaribu kuudaka badala yake ukamgonga na kutinga nyavuni

90' Kipenga kinapigwa kuashiria tamati ya mchezo, Coastal inafanikiwa kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara huku Pamba ya Mwanza nayo inasalia ligi daraja la kwanza.
 
Mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima si ilipigwa marufuku na Serikali? Au wanacheza bila Watazamaji uwanjani?
 
Refa anaibeba coast kwa nguvu zake zote Ila Pamba Inabidi waombe Sana Mungu, maana refa anaweza akazidi kutoa penati dhidi yao.
 
Coastal Union wanajua kuwakamia tu Yanga na Azam!! Wakicheza na timu nyingine, wanakuwa mdebwedo tu. Wamebebwa na mwamuzi lakini bado mchezaji anapiga penati kama mtoto wa primary vile!

Wakishuka daraja sawa tu hata kama na wenyewe ni Wagosi wa Kaya kama mimi.
 
Back
Top Bottom