NMDA antagonist
Senior Member
- Mar 25, 2018
- 149
- 106
UNAMFAHAMU HAMZA BENDELLADJ?
Kabla sijakufahamisha kuhusu huyu Kijana Naomba kuulizia swali, kumuibia mwizi ni kosa? Na je kuiba na kugawa kwa wahitaji ni kosa au laa... Majibu ya maswali hayo yatahitajika sana katika kuamua hili!
Maarufu Kama mwizi mwenye tabasamu "Smiling Hacker" Hamza Bendelladj ni kijana wa Ki-Aljeria aliyesumbua sana taifa la Marekani na nchi za Ulaya. Alizaliwa tarehe 1 January 1988 na kupata degree ya computer science.
Kijana huyu alitengeneza program ya computer inayofanya kazi kwenye windows inayojulikana kama SpyEye, ambayo ni kirusi kinachoweza kuiba taarifa za kibenki hivyo kumwezesha kufanya miamala batili kutoka akaunti za watu mbalimbali.
Aliweza kuiba pesa kutoka takriban benki 217 za USA na nchi za Ulaya kama Ufaransa, kiasi kinachokadiliwa kuwa $ 4 billions, ambazo alizigawa kwa mashirika ya kusaidia jamii Afrika na Palestina, ikiwa pesa nyingi zaidi aliyapatia mashirika kutoka Afrika na $280mils aliyapatia mashirika ya Palestina.
Mbali na hilo alidukua system ya kutoa Visa ya Ufaransa akawapatia Visa vijana wa Algeria waliokuwa wanahitaji visa ili waweze kuingia Ufaransa.
Pia alidukua tovuti ya serikali ya Israel na kuweka ujumbe uliokuwa unapinga Israel kukalia maeneo ya Palestina.
Alikuwa kati ya mahacker 10 waliokuwa wakitafutwa na alikamatwa akiwa Thailand akapelekwa Marekani kujibu mashitaka. Hamza alianza kutafutwa baada ya kujulikana pale alipomuuzia copy ya SpyEye agent wa CIA aliyejifanya naye ni hacker.
Israel ilimtaka akaisaidie kutengeneza upya system yake ya tovuti zake ili zisidukuliwe kwa ahadi kwamba serikali ya Marekani itafuta mashtaka yake lakini Hamza alikataa kufanya hivyo wala kutoa ushirikiano.
Baada ya kufikishwa mahakamani alikadiriwa kupewa kifungo cha miaka 65 jela na faini ya USD 14 Million, alikubali mashtaka na kupunguziwa adhabu mpaka miaka 15 jela.
Alipewa Jina Happy Hacker Kutokana na kwamba alionekana akitabasamu muda wote. Mwaka 2015 kulizuka uvumi kuwa Hamza Bendelladj amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa na picha "zake" kusambaa katika mitandao ya kijamii kitu ambacho kilikanushwa na serikali na kwamba picha zilizokuwa zikisambaa zilikuwa ni za Kijana aliyekuwa akifanana naye aliye hukumiwa na kunyongwa huko Tehran Square kwa kosa la mauwaji ya Jaji Hassan Maghaddas aliye uwawa miaka miwili nyuma, Kijana huyu aliitwa Majid Kavousifar.
Huyu ndiye Hamza ambaye kwa wengine wanamuona shujaa wakati wengine wakimuona mwizi.Aliwahi kusema kuwa yeye haoni maana ya kuwa na pesa nyingi wakati kuna watu wana uhitaji wa pesa kwa ajili ya chakula.