Pingania haki ya maisha yako

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,914
AINA YA MATESO; FAIDA NA HASARA

Nawashukuru walioungana nami kwenye ukurasa huu, nawaomba tumalizie somo letu kwa kuangalia vidokezo vichache vilivyosalia.

MATESO YA KUTETEA HAKI;
Siku zote mtu anapoamua kuteseka kwa ajili ya kutafuta haki yake, huwa anafanya kitu kizuri ambacho kitamfanya baadaye awe shujaa mbele ya jamii au hata kwa nafsi yake mwenyewe. Kuna watu ambao wamedhulumiwa haki zao, wanaonewa katika hili na lile lakini wanashindwa kupigania haki kwa sababu wanaogopa gharama za mateso. “Siwezi kushindana na mtu mwenye uwezo.” Kutokuweza kupigania haki kwa kuogopa kuteseka ni kujipa mateso mengine makubwa zaidi ndani ya nafsi yako, kwa sababu kila siku utaendelea kuumia, kulia na kulalamika kudhulumiwa haki yako, jambo litakalokufanya utetereke kiafya na hasa akili. Wanasaikolojia wanasema, ni bora kutesekea haki yako hadi hatua ya mwisho kwani itakusaidia kukuondolea mawazo ya kinyonge ambayo ni mabaya zaidi.

KUTESEKA KWA AJILI YA KUPATA MAENDELEO;
Maendeleo hayapatikani kwa njia za mkato, watu wengi tunaowaona wameendelea, historia zao zinaonesha kwamba, waliteseka sana kufikia hatua ya mafanikio. Kwa wale ambao wanatambua mchango wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, pamoja na mafanikio yake, wafuatilie historia ya maisha yake kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda linalotoka kila siku ya Jumatatu, wataona jinsi alivyoteseka katika kutafuta mafanikio Unapoamua kujinyima katika jambo fulani, kuishi maisha ya dhiki, kula kwa tabu kwa lengo la kutafuta mafanikio, faida yake kubwa ni kuyafikia malengo yako na kuishi kama mfalme katika siku za usoni.

KUTESEKA KWA KUKOSA MAARIFA;
Wapo watu ambao maisha ya ndoa ni magumu sana kwao. Kila siku ndoa zinawatesa, si kwa sababu wao wana ndoa za tofauti na binadamu wengine la! Ni kwamba, wamekosa maarifa ya kuwafanya waishi kwa amani. Kuna wengine mateso yao yapo kwenye utaratibu wa kuishi, utakuta wanajikwaa sana katika mambo ya bahati mbaya, mara wamepata janga hili, mara lile lakini ukichunguza kwa makini utagundua kuwa, wingi wa mateso yao unaletwa na kukosa maarifa ya nini wafanye na kwa wakati gani? Inakuwaje mtu unakunywa pombe nyingi kupita kiasi halafu unaendesha gari hovyohovyo hatimaye unapata ajali na kujisababishia majeraha au kuharibu gari na kutumia pesa nyingi kulitengeneza wakati ungetambua kipimo cha ulevi wako na kunywa kwa staha ungeweza kujiondolea mateso yasiyokuwa ya lazima. Hakuna kitu muhimu katika maisha kama kujielimisha namna ya kuiishi duniani. Ulimwenguni kuna mambo mengi, jaribu kila siku kujipatia elimu ya jinsi ya kuishi na wenzako bila migogoro, kila kitu ambacho hukifahamu vizuri jifunze hata kupitia kwa wenzako ili usiendelee kuteseka kwa vitu unavyoweza kuviepuka kwa kutumia akili za kawaida.

Naamini nitakuwa nimeeleweka vizuri kwenye somo hili. Nikutakie mema wewe msomaji wangu katika mwaka huu wa 2017 ambao ni mwaka wa namba isiyogawanyika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom