Pinda aumbuliwa bungeni

Niliisikia hii hoja jana bungeni kwenye Q&A sesion, imekuwa kawaida ya viongozi wa serikali kuomba ushahidi kutoka kwa mlalamikaji, hii ni tabia ya kukwepa majukumu na kutjiamini ktk utendaji, shahidi nyingi zimeshawasilishwa lakini matokeo hayatolewi. Mfano, Ushahidi wa Godbless Lema dhidi ya PM, Ushahidi wa Zito Kabwe juu ya CHC kuingiliwa na Waziri fedha nk.
 
Si afadhali za pinda zinafahami zinakwenda wapi, zile zinazochangishwaga kwenye mikutano ya kampeni kwa bakuli huwa zinakwenda wapi jamani?
Yale mafuta ya magari ya msafara yananunuliwa na nini.
 
 
kwani hao mbuzi wanapelekwa wapi.? Dar ,mpanda au wanauzwa anarudishiwa pesa.?
 
Kengemumaji, kuchangia kwa hiyari hakuna tatizo. soma historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Mwl Nyerere alikuwa akipanda ndege kwenda UN kwa fedha zilizochangwa na watanganyika. Historia inajirudia, tunapoelekea ukombozi wa Tz watu wanahiyari kuchangia harakati hizo.
 
huyu pinda nae na vijizawadi vya mbuzi ndo nini sasa?? washamuona ni mtu wa njaa njaa sana ndo maana wanampa vimbuzi au?? mnatutia aibu viongozi wa juu wa taifa hili...
 
Hizi nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya wa kuteuliwa zifutwe. Hazina Tija.
 
Pinda mzee wa meeeeeeeeeeeeeeeeee.

Jamaa Agrey alitokwa na povu utafikiri alikuwa anataka kupigana,yaani ailipanic sana.
Nafikiri hii zawadi haikuwa ya pinda peke yake.
 
Pinda ameipindisha sana hii nchii, tukiongea anaanza kulia...
 
kila mbuzi hula kulingana na urufu wa kamba yake , je akienda mikoa ya kusini lindi/mtwara atakusanya kuku?
 
We mzima kweli.....?eeemungu tusaidie
Hivi hili lina tofauti gani na lile la baadhi ya vyama vya siasa kuwakamua wapiga kura kwa kutembeza bakuli eti kwa madai kuwa hawana pesa, wakati tunajua wazi kuwa vinapata ruzuku, misaada toka ndani na nje ya nchi na vyanzo vingine vyingi.
 
Hivi vichwa vya habari vyengine vimekaa kiudaku. Hili la Mkuu wa Wilaya kuchangisha mbuzi "kwa ajili ya Pinda" linamhusuje Pinda? Hatuoni kama viongozi wengi walafi hutumia jina la kiongozi wa juu yake kwa maslahi yake binafsi? Hivyo "vijizawadi" vinavyokusanya huishia kama ngawira katika matumbo ya wenye njaa. "Mgeni njoo mwenyeji apone.

Kitu kingine ningependa kukigusia, ni kwa nini wabunge wetu wa upinzani hawajifunzi na mbinu chafu za CCM? Tayari wanaelewa wazi kuwa taarifa yoyote inayowagusa CCM ikipelekwa bungeni "lazima upeleke ushahidi", kwa hivyo kwa nini mbunge anasikia habari tu ndani ya TV na kufanya kuwa ndio ushahidi wake? Ingekuwa vyema kwa mbunge mtoa hoja kukusanya ushahidi wa kutosha, kama vile kwenda kunakohusika, kukutana na waliosekwa ndani, kwenda walikosekwa n.k., kuliko kuanza kutafuta ushahidi huo sasa ambapo tayari wahusika wataanza kuficha takataka zao chini ya mazulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…