Ningependa kusahihisha statement yako. Katiba inasema hivi:
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na
ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
walio wengi.
Hivyo basi, it's clear kwamba Rais ndo anayemchagua waziri mkuu na Bunge ndo linalomthibitisha. Na sio Bunge kumchagua.
Anyway, ndo hapo sasa tunataka kuleta mchezo wa Kenya na Zimbabwe. Sasa inaponoga zaidi ni hapa:
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Kwa hiyo basi, serikali inaongozwa na Rais, full stop. Sasa kweli itawezekana kuwa na serikali iliyoundwa na vyama viwili?