Mbasembase1970
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 6,056
- 4,608
Hili la picha za "kudhalilisha" za Waheshimiwa Wateule lituachie funzo Wanajamii
Jamii yetu imejikuta kwenye mjadala mkali baada ya baadhi ya Waheshimiwa Wateule picha na video zao za utupu (zisizo na staha) kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku jamii ikihoji kuhusu maadili yao.
Ndio, Jamii inahoji kwa sababu hao sasa ni viongozi wa Umma, ni mali ya Umma, Umma unahoji maadili ya viongozi wao.
Kimsingi kiongozi ni Kioo cha Jamii, yeyote mwenye ndoto za kutaka kuwa kiongozi lazima ajue kuwa anataka kuwa kioo cha anaowaongoza. Atake asitake watu watajitazama kutoka kwake.
Hivyo matendo na matukio yake yanapaswa kuzingatia kuwa ipo siku watu watajitazama kutoka kwake. Kiongozi hana faragha binafsi, ni mali ya umma. Kwa nchi zenye misingi imara ya kimaadili, maisha binafsi yanaweza kuwa sababu ya kukupandisha au kukuporomosha.
Tuachane na Wateule.
Je, sisi wana jamii kuna lolote tunalojifunza kutokana na kusambaa kwa picha hizo? Lipo.
Mitandao ya kijamii imeingia kwenye jamii yetu miaka ya 2000's wengi wetu mpaka leo hii bado hatuna weledi (ufahamu) mzuri wa namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii. Hasa ni nini tunapaswa kupost kwenye mitandao na nini hatupaswi kupost.
Wengi tunadhani kuwa kwa kuwa simu, tarakilishi au tarakilishi mpakato ni mali yetu hivyo tunao uhuru usio kuwa na mipaka wa kupost chochote tunachojisikia kupost. Hapa wengi tunakosea kwa kuamini hivyo.
Bahati mbaya sana Dada zetu wamekuwa ndio wahanga (victims) wa kinachoitwa picha za kudhalilisha mitandaoni. Sababu zipo wazi Dada zetu wengi wamekuwa na kasumba ya kupenda kupiga au kupigwa picha zao na kupost mitandaoni. Kwao ni jambo la kufurahisha, kujitambulisha, kuhabarisha, kujitanabahisha, kujifaragua, kujinadi, kujiuza n.k
Mtandao jamii wa Instagram ni kinara kwa picha nyingi za utupu za kinadada. Ni kama vile wanashindana nani atapiga picha ya utupu zaidi na kuipost mtandaoni. Ukiachilia wale wanaopiga na kupost kwa malengo ya kujiuza (dadapoa), wako kundi la wanaojiita wanamitindo (fashionist), wako kundi la wauza sura (video vixen), wako wabunifu mavazi (designer), wako wajasiriamali (entrepreneur) na wako kina mwenzangu na mimi ambao wao ni bendera fuata upepo ambao wanapoona wenzao wamepost nao bila kujiuliza kwa nini hawa wamepost hivi hudhani labda ndio fasheni basi nao hupiga na kupost, wanaiga kila kiingia mjini.
Hali hii ndio inasababisha dada zetu wengi kujikuta ni wahanga wa picha za kudhalilisha mtandaoni pale ambapo picha walizopiga na kuzipost wao wenyewe pasina kujua madhara yatakayotokea baadae endapo zitachukuliwa na kusambazwa zaidi mitandaoni. Wanaume japo wapo pia mitandaoni lakini kwa kiasi kikubwa sio waathirika sana wa udhalilishaji wa picha za mitandaoni ukilinganisha na wanawake.
Sheria namba 14 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 (The CyberCrimeAct No. 14 of 2015) ibara ya 14 inakataza mtu yoyote kutuma (post) au kusambaza (repost) picha yenye kuashiria Uasherati (pornography) na adhabu kubwa zaidi iliyotajwa kws makosa hayo ni kifungo gerezani kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milioni 30 au vyote kwa pamoja. Bahati mbaya sheria hii haijatafsiri wazi picha chafu ya uasherati maana yake ni nini.
Kupiga na kupost picha inayoacha wazi baadhi ya sehemu zako za siri kama mapaja, matiti, makalio, kiuno, tumbo, nguo zako za ndani, umbile lako n.k zinaweza kutafsiriwa kuwa ni kiashiria cha uasherati kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao au kulingana na jamii inayokuzunguka.
Hivyo umakini mkubwa sana unahitaji kwa mtu anapopiga na kupost picha ili isije kutafsiriwa kuwa ni picha yenye kuashiria Uasherati. Wadada wanapaswa kuwa makini sana kwenye nukta hii maana wao ndio wahanga wakubwa, kama sio kukamatwa na kuhukumiwa kisheria basi picha zao zinaweza kutumika kuwadhalilisha au kuwakejeli kama ilivyotokea kwa baadhi ya Waheshimiwa Wateule.
Najua kuwa neno langu haliwezi kubadilisha chochote lakini ujumbe nimefikisha.
Kama una ndoto za kuwa Kiongozi wa umma basi fahamu kuwa wewe ni Kioo kitarajiwa cha Jamii, hauna tena maisha yako binafsi, watu watajitazama kutoka kwako. Usije kulalamika ukaona unadhalilishwa kwa kazi za mikono yako mwenyewe. Utapata tabu sana.
C&P from facebook

Last edited by a moderator: