Mstaafu Rais Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa Mei 8, 1925) akiongoza matembezi ya kilometa 5 ya hisani ya 2014 Dar Rotary Marathon ambapo waandaaji, Klabu ya Rotary walifanikiwa kukusanya takribani shilingi milioni 500 na ahadi ya shilingi milioni 300/- kwa ajili ya hatua ya pili ya jengo la kisasa la ujasiriamali na kituo cha taarifa-mali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitakachogharimu shilingi milioni 400/-. Pichani Rais Mwinyi anaongozana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kushoto kwake) na Meya wa Manispaa ya Kindoni, Yusuph Mwenda.