picha ya nyalandu na wachina wa kariakoo imefikia........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

picha ya nyalandu na wachina wa kariakoo imefikia........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Jun 24, 2011.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Heshima wakuu!
  naandika nikiwa na kumbukumbu ya senema ya mchanganyiko wa vionjo vya kibongo na kichina (kichibong) ambapo mhusika mkuu akiwa waziri mdogo wa viwanda na biashara ........... NYALANDU.
  Alituambia mchana kweupe anawatimua wamachinga wa kichina (nadhani kwastaili za kibanga) anapenda kusema "ili kuhakikisha kwamba........" wanabaki wawekezaji wenye sifa na hadhi ya kiwekezaji. kwa waliopita kariakoo hakuna dalili ya wataalamu wa kunk-fu bin shotokan kuonekana kiwekezaji zaidi kuliko kimachinga, tumeliwa!!!!
  hakuna mchina ambaye amepandishwa pipa kurudishwa gwang-zu,
  Naazimia kusema NYALANDU ni muongo, kaliongopea taifa, anatumia vibaya fedha za umma kujitafutia umaarufu wakisiasa, hana nia njema na nchi yetu, kwa anayedhani au kuamini namsingizia NYALANDU amwage utetezi wake humu jamvini.
  Nawasilisha
   
 2. PongLenis

  PongLenis JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hahaha na je wabongo walijaa huku Guangzhou na yiwu .. warudishwe bongo..?! wapo wanafanya hadi biashara za baba lishe huku .. mkiwapandisha pipa na wao watawapandisha pipa huku na kuwapa hadhi ya wanigeria kwani so far huku tuliko mchina anathamini mwenye passport ya tzn kuliko ya wanigeria.. kuna siku askari walikuwa wakipita nyumba badala ya nyumba kukamata waafrica mamluki walipona wenye passport za BONGO tu!
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  ponglenis, kumbuka waziri alituaminisha kwa nafasi yake kuwa katika kuhakikisha kwamba masuala ya uwekezaji ni wawekezaji wenye sifa ya uwekezaji ndiyo wanafanya uwekezaji na si kufanya shughuli za ujasiriamali mdogomdogo wa kuuza karanga.
   
 4. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tusilalamike bure, tuchape kazi! Nimefika Italy, Lecce, nimekuta mtanzania ametandika toys n avikorokoro used anauza, from the way nilivyomuona kale ka-renault alikokashehenesha kila kitu ni kama ndiyo nyumba yake! Trust me, wako wabongo kule wanafanya vikazi vya ajabu! China wamemwagiga sana...tena siku hizi hata dada zetu wanakwenda kuuza China, Malaysia, UAE na Singapore...hawana work permit, wanaishi kiujanja ujanja tu! Nao vipi warudishwe?? Na wakirejea waje kufanya nini??
  Watanzania kibao wamejaa UK, USA, Germany etc. Wengi walikwenda kwa kusoma, wamemaliza shule lakini bado wanang'ang'ania huko! Wengi wao sasa wanafanya vibarua kule, kazi amabazo wenyeji wangeweza kuzifanya....Tuwalalamikie hao nao ili warejeshwe?? Wakirudi Bongo watafanya nini? Kazi hakuna, umeme hakuna, maji hakuna, hela hakuna........!
  Waacheni wachina wa watu, wamejikita huku kwa kuwa sisi wenyewe ni mabwege, ni serikali iliyowakubali sasa nini tena? Wenzetu wanaweka vigezo vy akuingi anchini kwao kuwa vigumu, na ada ya kulipia work permit ni kubwa...kuongeza revenue, lakini sisi sijui ni dola 50?? unategemea nini>??
  Nyalandu ni kama Pinda na Kikwete....ndiyo CCM yenu hiyo! Hatutakaa na kuona mambo yako sawa hata kidogo
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Tatizo nyalandu inaonekana ana washikaji zake pale kariakoo ambao ndio walikuwa wanampa kero zao kwa vile wanavyo compete na wale wachina katika kusaka noti,sasa ule mziki nyalandu akauingia kizembe akidhani ni mdogo kivile, jamani tusidanganyane ule mziki mzito kama ni kuingia chaka basi tumesha ingia na kama ni kuwatimua basi na wahindi tuwatimue. Mbona wahindi wamejazana mpaka sasa wanaitunishia misuri serikali kuilazimisha iwauzie nyumba zetu sisi watanzania. Hapa ofisini kwangu siku moja kapita mchina nikawa napiga nae story badae nikachomekea hilo, kwanza alianza kwa kucheka kicheko ambacho kilionesha dhahiri kuwa anamshangaa nyalandu kwa kutaka sifa, aliniuliza mbona wahindi ni wengi na hamuwafukuzi? akaniuliza ivi kati ya china na india ni nchi ipi inayotoa misaada ya nguvu kuiendeleza tz, akauliza pia ivi kuna dhambi kwa mchina kuja kufanya biashara tanzania? akauliza wale wachina walioko pale kariakoo hawajatoa ajira? na mwisho akauliza ivi wale wachina kariakoo hawalipi kodi? nilimjibu maswali yake yote lakini alinishinda kwa hoja nikaachana naye
   
Loading...