Picha ya leo

Hivi sisi kweli kwa namna yoyote ile viongozi wetu wanatuonyesha namna ya kupambana ili kurahisisha maisha yetu? Mi naona wanapambana ili kurahisisha maisha yao tu.
Tatizo la hapa nchini kwetu ubinafsi umebadilika na kuwa sifa njema katika jamii!
 
mkuu ukiondoka nyumbani kwako usipende kuuliza mambo ya nyumbani!
Kwa mfano mtoto angekujibu kuwa mama bado amelala na baba mwingine,kazi zako ungeendelea nazo?

Nataka nijue hali yake mkuu
 
Tatizo la hapa nchini kwetu ubinafsi umebadilika na kuwa sifa njema katika jamii!

Ya hii inatu cost sana. Zamani kiongozi akiingia alikuwa anawafikiria watu anaowaongoza lkn viongozi wa siku hizi kuanzia rais mpaka shina wakipata madaraka wanafikiria kuchumia matumbo yao na familia zao tu. Zamani uongozi ulikuwa ni hazina siku hizi mbunge akipata ubunge anasema hata nisipopata tena poa tu coz ana uhakika hawajali wananchi waliomchagua
 
Tukiendelea na tabia hii,basi maendeleo makubwa tutakuwa tunasikia kwa wenzetu tu!
 
Mkuu tunachotaka tunakijua,tatizo letu kubwa ni ubinafsi!

hata hizo ngozi nyeupe zina ubinafsi, ila wanajua wanachofanya when it comes for the future generations na for the matter of national interests
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…