Nyumba ipo Kivule mwisho ( Gongo la mboto jijini Dar es salaam ).
Nyumba ina sieating room,
dinning room,
choo ndani,
na jiko
.Pia ina vyumba vitatu vya kulala ambapo kimoja ni master room.
( ZINGATIA ) Nyumba hii bado ujenzi haijaisha hivyo inauzwa kama ilivyo. Madirisha yote yameshawekwa. Milango mikuu yote tayari imeshawekwa mageti. Choo cha public tayari kipo na sink. Makalo ya maji taka yapo na yameshakamilika. Baadhi ya milango ya ndani tayari imeshawekwa fremu mingine bado.
Hakuna shida ya maji
Gari linafika hadi nyumba ilipo pasipo shida yoyote
Umeme haupo mbali kabisa
Bei ni Milion 22 ( maongezi yapo )
Kwa aliye-interested tuwasiliane 0715553166
Kuwa specific, ni kivule au gongolamboto? Taja eneo halisi nyumba ilipo na ikiwa haina mgogoro wowote au ikiwa haipitiwi na mradi wowote wa serikali.
hakuna picha
duh, nina hofu na hiyo bei, naona kama ipo chini sana, ukiangalia nyumba na bei nahisi harufu fulani hivi....nawatakia mema wanunuaji. sijui lakini.
Nyumba ipo Kivule. Unapanda gari liendalo Gongo la mboto then unashuka kituo kiitwacho Banana. Hapo Banana utakuta daradara zinakwenda kivule na utashuka mwisho wa gari yaani Kivule ccm. Baada ya hapo ni hatua kadhaa tu umefika kwenye nyumba. Nyumba haina mgogoro wowote. Na hakuna mladi wowote wa serikali unaopita. Ondoa hofu kabisa. Tuwasiliane hapa 0715553166
Mkuu hata mimi nina doubt.Lakini ni vyema mnunuaji uende mahakamani.
Je INA hati
haina issue ya mirathi kweli maana sijui kwa nini nimeona huruma kwa huyo dada na huyo dodo halafu hiyo bei sasa mbona siyo?
Kaka maisha ni kupanda na kushuka. Na wakati mwingine mipango ya mtu huenda tofauti na vile alivyopanga. Nyumba yangu naiuza siyo kwa kupenda bari ni shida tu. Nahitaji kiasi fulani cha pesa haraka. Na hii siyo nyumba ya urithi. Hii ni nyumba ambayo nimejenga mimi na mke wangu na leo kwa pamoja tumeamua kuuza. Atakaye afiki kutoa hiyo milion 22 hata kesho tu namuuzia nyumba na atanikumbuka naamini. 0715553166