Picha: Madhara ya Magufuli Kuwatishia Wakuu wa Wilaya/ Mikoa

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,936
Wakuu,
Katika hotuba yake na "Wazee" wa Dar, Rais Dr. John Magufuli alitoa tamko kuwa amechelewa kuteuwa wakuu wa Mikoa na wilaya mpaka hapo atakapojihakikishia kwa hawa waliopo kuwa wanaendana na "Kasi" yake.

Isitoshe, Rais alimpongeza Mh. Makonda na kumhakikishia kuwa atakuwepo katika teuzi hizo iwe kwa cheo hicho au kupanda cheo na "wengine" wasimwonee "gere" au wasishangae! Paul Makonda ametumia vyema media house ya clouds kuweza kupata attention ya kutosha Ikulu na hata kwenye vyombo vingine vinavyoweza kuwa na ushawishi wa teuzi hizi, katika taarifa ya habari clouds tv makonda habari zake huwa chini ya theme "Ndoto kubwa ya Makonda Kinondoni", theme hiyo huja na taarifa yoyote inayomhusu DC huyo hata kama haina umuhimu sana.
Kasesela.jpg


Iringa labda kwakuwa hakuna media nyingi zenye coverage kubwa, DC wa huko Ndg. Kasesela yupo katika kampeni kubwa sana kupitia mitandao ya kijamii kuhakikisha anapata attention ya kutosha katika mamlaka za uteuzi. Picha hii inamuonesha Mh. DC akiwa amembeba mgongoni mtu mzima mwenye uwezo wa kuruka madimbwi kama hayo anayovushwa hata mia. Lugha ya picha inaongea maneno zaidi ya 1000...
 
Ni akili tu katumia kucheza na watu, anatumia media kujikuza lkn Kuna uwezo binafs kaongeza km ni media kwann wengine wasitumie hizo media, yeye amekuwa wa mbele kuhamasisha nichezo kwa vijana amekuwa akiongelea suala la ajira kwa ukaribh na wananchi wake lkn Zaid ya yote Makonda Ana mapungufu yake kama mwanadamu
 
Yaani hali ilivo ni kuwa sasa hivi wote wana ogopa basi ni fukuza fukuza hata kama mambo unaweza kuyamaliza kwa kuelekeza kuwa hutaki uzembe ..Juzi namuana waziri anashika fagio nae anapiga deki pale muhimbili...haya yote ni woga walio nao hawajiamini ..ni hatari lakini wanaweza kuvuka mipaka mfano makonda kuwatia ndani wale wafanyakazi wa ardhi
 
Back
Top Bottom