Phiri: Nasaini kuifundisha Simba leo tar5 December 2012


Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,913
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,913 2,000


Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Malawi (The Flames), Kinnah Phiri, amesema kwamba tayari ameshakubaliana na uongozi wa klabu ya Simba ili ajiunge na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na leo atasaini mkataba wa kuifundisha klabu hiyo ya Mtaa wa msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na NIPASHE jana, Phiri, alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoendelea jijini hapa, atasitisha mkataba wake na Chama cha Soka cha Malawi.


Kikosi cha kocha huyo kilitolewa jana katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kenya ‘Harambee Stars’.


Mchezaji huyo wa zamani wa Malawi alisema anaamini atakuwa na matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na anafurahi kusikia Simba ndiyo klabu yenye wachezaji wengi wanaozitumikia nchi zao.


"Nilikuwa nimeshaamua kupumzika kuiongoza Malawi, sasa nashukuru kupata kazi Tanzania na Simba ni moja ya klabu kongwe ambazo zinasaka mafanikio na mimi nitajitahidi kuifikisha huko," alisema kocha huyo.


Aliongeza kwamba yeye alikuwa tayari kujiunga na Simba tangu mwaka jana, lakini mazungumzo hayakukamilika na sasa ndiyo wakati muafaka umefika.


Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kwamba wameshakamilisha mazungumzo na Phiri na kilichobaki ni kusaini mkataba wake kabla ya kuanza kazi.


Kaburu alisema kwamba yeye pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspoppe, wanatua leo Kampala, Uganda kukamilisha mazungumzo na Phiri na kusaini naye mkataba, huku pia wakikamilisha mchakato wa kuwanasa nyota wengine wanaowahitaji.


Alimtaja mshambuliaji wa Express na timu ya taifa ya Uganda, Brian Umony kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuingia nao mikataba leo.


Aliongeza kwamba tayari wachezaji wengine wa Simba waliobakia Dar es Salaam wameshaanza mazoezi ya viungo na baadaye watahamia ufukweni baada ya wiki mbili kumalizika.

CHANZO: NIPASHE
 
PrN-kazi

PrN-kazi

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Messages
2,901
Points
1,225
PrN-kazi

PrN-kazi

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2011
2,901 1,225
....si dhani kama huo Phiri wa Malawi atakuja na jipya sana ndani ya Simba: zaidi ya walivyokua makocha waliopita ndani club kama vile akinaa:-James Sian'ga, Phiri wa Zambia, Julio 'Mtz mtaalamu' na Milovan a.k.a Prof.
 
Aggrey86

Aggrey86

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Messages
855
Points
195
Aggrey86

Aggrey86

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2011
855 195
Dah! Kwa hiyo Prof.ndo kweli harudi jamani dah! Soka la bongo makocha inabidi wawe na moyo mgumu kama makocha wanaoenda kufanya kazi Chelsea!
 
stevelwa

stevelwa

Member
Joined
Nov 2, 2012
Messages
72
Points
0
stevelwa

stevelwa

Member
Joined Nov 2, 2012
72 0
Karibu phiri, huku tanzania hususani mpira ni ajira. Ukipiga marekodi mazuri utadumu, ingawa prof milovan hajatendewa haki, ila tusubiri tuone hayo.
 

Forum statistics

Threads 1,283,748
Members 493,810
Posts 30,799,708
Top