Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Leo tarehe 28/01/2017 tulikwenda kumtembelea na kumfariji mbunge wa Jimbo la Kilombero kamanda Peter Lijualikali (Mb) anayetumikia kifungo cha miezi sita jela. Yupo IMARA sana!
Ametupokea kwa tabasamu na bashasha nyingi. Katika maongezi yetu, alituachia ujumbe mzito sana kwa wabunge na wapenda haki wengine;
"Lakini makamanda acha niwaachie ujumbe mmoja mpeleke kwa wabunge wenzangu, wasijione waheshimiwa sana. Mimi hapa nimechanganywa na wafungwa wa kawaida tu, ninakula chakula cha mawe na kufanya kazi kama mfungwa mwingine wa kawaida. Ubunge hautambuliki kabisa hapa. Wakati haya yakitendeka, wezi wa pembe za ndovu na wauza madawa ya kulevya, wamewekwa VIP na wanakula special diet. Mimi walaah nawaambia sitaweka bendera ya bunge tena kwenye gari yangu"
Mengine nayahifadhi lakini inakera na kutia hasira sana.