Jamani naombeni kuuliza kuna watu wanagawa pesa mitaani wakidai ni pesa za TASAF kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza yaani kaya maskini pesa hizo zimesambazwa kwenye maeneo ya vituo vya Iliboru na Sanawari na wamepewa vijana wengi waliokuwepo maeneo yale na kila mmoja alipata kiasi chake kuna waliopewa elfu 30 wengine elfu 40, 50 na wengine laki moja moja.
Jamani inakuwaje pesa za watu wasiojiweza kuja kugawanywa kwa vijana mitaani tena wanaokunywa viroba kupindukia kwanini wasingechunguza hizo familia maskini na kuwapatia msaada wa kiuhalali tena pesa zenyewe zimeletwa kwa kushtukiza.
Inakuwaje watu wanajitokeza unaona kabisa huyu ni mzima lakini bado unampa laki moja kama hayo majina ya wanaostahili kupata hizo pesa hawakuwepo karibu kwanini zisingerudishwa na kuandaliwa utaratibu upya?
Si bora wangezirudisha hizo pesa zifanyiwe kazi nyingine au ziende hata kwa watu wengine wenye shida? si kuna watu kila siku wanatangaza kwenye vyombo vya habari ITV, TBC wakiomba msaada wa kuwatibu ndugu zao kwenye hospitali za ndani na nje ya nchi yetu kwanini wasingepata mgao huo?
Kwa kweli utaratibu wa ugawaji wa pesa hizi haukuwa wa halali tena zinagawanywa chini ya ulinzi wa askari jamani hizi pesa zimezua mjadala hadi wengi wamefikia hatua ya kujiuliza ni rushwa ya uchaguzi mkuu ujao? au ni za matambiko? manake hazijawafikia wale walengwa ambao wamekusudiwa nini kinaendelea au kuna siri gani ndani ya huu mgao?