Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,086
- 1,081
PESA YA RADA
PESA YA BUNGE
TANGAZO LA TAMISEMI
============
1. Pesa za rada zilitengeneza madawati mangapi, shule zipi zilipokea hayo madawati na vitabu.
2. Pesa za bunge tumeambiwa inatosha kutengeneza madawati 120,000, je madawati hayo yatapatikana?
3. Simbachwene ametua agizo kila halmashauri iwe imetengeneza madawati ya kutosha na asiwepo mwanafuzi wa kukaa chini, ametoa agizo bila ya halmashauri hizo kupewa pesa za kufanyia kazi.
Halmashauri wameanza kutengeneza madawati kwa kuzuia pesa za likizo na matibabu kwa watumishi wake, itakuwaje kama madawati ya bunge yatatengenezwa kwa idadi ya 120,000 hayo madawati yatapelekwa wapi?
ZAIDI ya shilingi bilioni 72 zilizorudishwa kutoka kwenye “chenji” ya rada zimeelekezwa kwenye kusaidia malengo ya Wizara ya Elimu na Ufundi katika kiwango cha elimu ya msingi.Hususani manunuzi ya vitabu na madawati katika shule za msingi Tanzania Bara.
Pesa hizo zililejeshwa kutoka kwenye malipo ya ziada yalifanywa na serikali kinyume na utaratibu kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza katika manunuzi ya rada.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Zitto Kabwe alitaka kujua, "Pesa ya rada ilirejeshwa lini? Ilibadilishwa lini toka kwenye paundi kwenda kwenye shilingi za kitanzania?"

April 11 2016 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa ‘Takukuru’ na hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo, ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.
Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amewataka Watendaji wa Mamlaka zilizo chini ya Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa katika kipindi kijacho cha miezi sita, tatizo la upungufu wa madawati kwa wanafunzi shuleni liwe limemalizwa.