Peru yamtaka Trump kumsalimisha rais Toledo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_94278337_53e35aba-14de-4534-9093-9a74ce75719a.jpg


Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski ametoa wito kwa rais wa Marekani Donald Trump kumsalimisha rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo ambaye anatakiwa kujibu mashtaka nchini Peru.

Bw Toledo, ambaye inaaminika kwa sasa yupo mjini San Francisco, anatuhumiwa kupokea rushwa ya jumla ya $20m (£16m).

Amekanusha tuhuma hizo.


_94278340_6e6732bd-7a01-489a-9d34-c8c8d8b78d7b.jpg

Kupitia njia ya simu Jumapili, Bw Kuczynski alimuomba Bw Trump "kutathmini" hali hiyo. Kufikia sasa, juhudi za kumkamata Bw Toledo zimekwama kutokana na changamoto za kisheria.

Marekani imesema haiwezi kumkamata kiongozi huyo wa zamani hadi maelezo zaidi kuhusu kesi inayomkabili yawasilishwe kwake na maafisa wa Peru.

Maafisa nchini Peru, ambao waliomba akamatwe wiki iliyopita, wanahofia kwamba huenda akaondoka Marekani na kwenza Israel.

Hata hivyo, Israel imesema haitamruhusu kuingia nchini humo.

Bw Toledo kwa sasa ni profesa mgeni katika Chuo Kikuu cha Stanford.

Mkewe Eliane Karp, ana uraia wa Usrael.

Bw Toledo aliongoza Peru kuanzia 2001 hadi 2006 na ametuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil ya Odebrecht ndipo asaidie kampuni hiyo kupata kandarasi ya kujenga barabara kuu ya kuunganisha Peru na Brazil.

Zawadi ya $30,000 (£24,000) imeahidiwa yeyote atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa kwa Bw Toledo.

Wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema Bw Toledo hataruhusiwa kuingia nchini humo hadi "masuala yanayomhusu Peru yahitimishwe."

_94278342_d5f59b74-ba20-4041-90f8-4a870309eff1.jpg
 

Attachments

  • _94278340_6e6732bd-7a01-489a-9d34-c8c8d8b78d7b.jpg
    _94278340_6e6732bd-7a01-489a-9d34-c8c8d8b78d7b.jpg
    28.2 KB · Views: 38
Back
Top Bottom